PRODUCER MAN WALTER KUANZA KUTOZA MILIONI MOJA KWA NYIMBO MOJA

Man Walter 1

Man Walter

Mtayarishaji mahiri wa muziki hapa Bongo, Man Walter ametangaza kupandisha gharama za kurekodi nyimbo katika studio zake za Combination Sound kutoka gharama alizokuwa akitoza hapo awali hadi kufikia shilingi milioni moja.

Man Walter amesema ameamua kufanya hivyo kutokana na kwamba siku zimezidi kwenda na bei za kurekodi zimekuwa zile zile   huku wao watayarishaji wakibaki wakiwa wamedumaa wakati wasanii wanafanikiwa kuliko wao na kudai kuwa hajafanya hivyo kwa sababu ya wivu kwa wasanii bali ni katika kutaka kupiga hatua nyingine mbele kimaisha..

 Ili ufanikiwe kuna vitu ambavyo unatakiwa uchukue risk, bila kuogopa nini kitatokea, kama wasanii hawata kwenda kurekodi kwa sababu bei imepanda ni sawa lakini yeye anategemea ubora wa kazi anaoufanya kwaiyo anaamini anaweza kuendelea kufanya vizuri katika kiwanda cha muziki”, alisema Man Walter

Aliongeza :”soko lolote lenye bidhaa bora na kama wewe mfanyabiashara unaamini bidhaa yako ina ubora na soko huria unaweza kuweka bei unayoitaka na mteja anayehitaji bidhaa bora atakuja tuu kwako.  Wasanii watakaokuja na kufikia malipo hayo ya milioni moja atafanya nao kazi”.

Man Walter ambaye amefanikiwa kutwaa Tuzo za Kili mara mbili mfululizo kama mtayarishaji bora wa mwaka, anasifika kwa  kutengeneza ngoma kali zinazotokea kuwabamba mashabiki ikiwemo Baadae na Tupogo za Ommy Dimpoz, Dushelele na Mwana za Ali Kiba na ngoma nyingine kibao.

 

 

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s