WATIMANYWA AUNGA MKONO KUSIMAMISHWA SHINDANO LA MISS TANZANIA

Happiness WatimanywaMlimbwende wa Tanzania mwaka 2013, Happiness Watimanywa ameunga mkono kusimamishwa kwa shindano la Miss Tanzania akisema ni kweli shindano hilo lina mapungufu mengi yanayohitaji kufanyiwa kazi.

Watimanywe ambaye amerejea nchini mwezi uliopita akitokea kwenye shindano la urembo wa Dunia, amesema ni kweli wadada wengi wataathirika kutoka na shindano hilo kufungiwa lakini inabidi wakubaliane na ukweli ulivyo.

Watimanywa anadai kipindi akiwa kwenye kambi ya Miss Tanzania, alishuhudia madhaifu lukuki katika shindano hilo hivyo amefurahishwa na hatua ya baraza la  sanaa Tanzania ‘BASATA’ kufungia shindano hilo ili kasoro hizo ziondolewe.

kufungwa kwa shindano, nadhani inasikitisha because inatoa opportunity kwa wasichana wengi lakini pia nadhani ni opportunity nzuri kwa sababu kuna mapungufu kadhaa”, alisema Watimanywa.

Aliongeza :”kama nilivyosema kwenye uandalizi kulikuwa kuna watu zaidi yangu, kwaiyo i think ni opportunity ya kurudi nyuma na kuangalia ni vipi ni  vitu gani tunaweza kuvi-push ili tuweze kufanya vizuri zaidi, not only on the international things lakini hata  hapahapa Tanzania”.

Watimanywa amewashukuru  watanzania wote ambao walichukua muda wao kutoa support kwenye mitandao ya kijamii kupigia kura kipindi alipokuwa akiwania Taji la mrembo wa Dunia nchini Uingereza mwaka jana.

Sababu ya hii press conference ni kutoa shukrani kwa watanzania wote ambao walichukua muda wao kutoa support aidha katika social media lakini pia hata katika harakati za kupiga kura..uuuummmhh!! kwa sababu kama mlivyosikia mmeona kwamba tumefika nafasi ya pili katika people’s Choice Awards na iyo haijawahi kutokea before”, alisema Watimanywa

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s