SEPP BLATTER APATA MPINZANI FIFA

Pichani ni Sepp Blatter na Prince Ali Bin Hussein

Pichani ni Sepp Blatter na Prince Ali Bin Hussein

Makamu Rais wa FIFA, Prince Ali Bin Hussein ametangaza kuwania urais wa shirikisho la soka Duniani ‘FIFA’ dhidi ya Rais wa sasa Sepp Blatter.

Akitangaza kuwania nafasi iyo, Prince Ali Bin Hussein amesema zama za mkanganyiko unaozunguka mchezo mzuri wa soka lazima ufikie kikomo.

Aidha amesema kuwa sababu ambayo imemfanya kuwania nafasi iyo ya urais wa FIFA ni kwa kuamini kwake kuwa kwa sasa ni muda muafaka wa kuingia katika michezo na kuongeza kuwa vichwa vya habari vinatakiwa kuwa soka safi na sio kuhusu FIFA.

Prince Ali mwenye miaka 39, atasimama kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao utakaofanyika Mei 29 mwaka huu ambapo Sepp Blatter atakuwa akiwania muhula wa tano kuongoza shirikisho hilo.

Pia Prince Ali alikuwa ni miongoni mwa wajumbe waliokuwa mstari wa mbele kushinikiza kufanyika uchunguzi kwa tuhuma za rushwa na ufisadi zilizotolewa na mchunguzi Michael Garcia wa marekani juu ya uwenyeji wa kombe la Dunia  2022 nchini Qatar.

 

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s