KESI YA SHEIKH PONDA ISSA PONDA YAPIGWA KALENDA HADI JAN.19,2015.

Sheikh Ponda Issa PondaKesi inayomkabili katibu wa Taasisi ya Jumuiya za Kiilamu,Sheikh Ponda Issa Ponda imetajwa tena leo katika mahakama ya hakimu mkazi Morogoro na kuahirishwa kwa mara nyingine mpaka itakapotajwa tena Jan 19, mwaka huu na kusikilizwa tena kwa siku mbili mfululizo Jan 26 na 27 mwaka huu.

Kundi la wafuasi wa Sheikh Ponda na baadhi ya waumini wa dini ya kiislamu walikusanyika kwa wingi katika mahakama ya hakimu mkazi Morogoro kujua nini hatima ya kesi inayomkabili katibu huyo wa Taasisi ya jumuiya ya kiislamu.

Katika kesi iyo upande wa utetezi wa Sheikh Ponda unaiomba mahakama ya hakimu mkazi Morogoro kufuta hati ya kesi inayomkabili mshtakiwa uyo ya kukiuka amri ya mahakama na kurejea hukumu iliyotolewa na mahakama ya hakimu mkazi kisutu jijini Dar es salaam.

Sambamba na ombi hilo upande wa mshtakiwa unaomba mshtakiwa apewe dhamana, ombi ambalo hata hivyo limepingwa na upande wa mashtaka kufuatia hati ya shtaka linalomkabili kwani wao wametuma ombi la kukata rufaa mahakama ya Kisutu kupinga hukumu iliyotolewa na jaji Shango hivyo kesi iyo imepangwa kutajwa na kusikilizwa upya.

Mara baada ya kusikiliza pande zote mbili hakimu mkazi wa mkoa wa Morogoro, Bi.Mary Moyo amekubali kei iyo kuoangiwa Tarehe mpya na kutajwa pamoja na Tarehe ya kuanza kusikilizwa ambapo itaikilizwa kwa iku mbili mfululizo ambazo ni January 26 na 27.mwaka huu huku ombi la kutolewa kwa dhamana kukataliwa kutokana na mkurugenzi wa mashtaka kuzia kutolewa kwa dhamana dhid ya mhtakiwa Sheikh Ponda.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s