RAIS KIKWETE AMUAPISHA RASMI MWANASHERIA MKUU MPYA WA SERIKALI

George Masaju

George masaju akiapa mbele ya Rais Jakaya Kikwete

Hafla ya kuapishwa kwa mwanasheria mkuu mpya wa serikali, George Mcheche Masaju aliyeteuliwa Januari 02 mwaka huu, imefanyika Ikulu jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali na watendaji wengine pamoja na familia.

Kabla ya uteuzi wake Bw.Masaju alikuwa Naibu mwanasheria mkuu wa Serikali ambapo pia amewahi kuwa mshauri wa sheria wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Mwanasheria uyo anajaza nafasi iliyoacha wazi kufuatia kujiuzulu kwa aliyekuwa mwanasheria mkuu wa serikali, Jaji Fredirick Werema kutokana na alichokiita kuchafua hali ya hewa baada ya ushauri wake katika suala la Tegeta Escrow kutafsiriwa visivyo.

Akizungumza mara baada ya kuapishwa mwanasheria mkuu huyo wa serikali amesema atatekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria na kuwasihi wananchi kuwa na imani na serikali yao.

Namshukuru mheshimiwa Rais na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwamba wameendelea kuona kwamba wana imani na mimi naweza kuisaidia tena Taifa letu katika nafasi hiyo ya mwanasheria mkuu wa serikali”, Alisema Masaju.

George Masaju1

Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Rais Jakaya Kikwete akisaini nyaraka baada ya kumuapisha Bw. Masaju Ikulu leo

George masaju2

Rais Jakaya Kikwete akimkabidhi nyaraka za serikali mwanasheria mkuu wa serikali, George Masaju baada ya kula kiapo

Wageni

Wageni waalikwa wakimshuhudia mwanasheria mkuu mpya wa serikali akiapishwa Ikulu jijini Dar es salaam

 

George Masaju3

Rais Jakaya Kikwete, Mwanasheria mkuu mpya wa serikali na viongozi wengine wa serikali katika picha ya pamoja

Mcheche Family

Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete katika picha ya pamoja na familia ya mwanasheria mkuu mpya wa serikali

 Picha kwa hisani ya Michuzi Blog

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s