RAILA ODINGA AFIWA NA MTOTO WAKE WA KIUME

Fidel Odinga

Pichani ni Fidel Odinga enzi za uhai wake akiwa nje ya kituo cha polisi cha Kabete May 25, 2011 akisubiria kutoa maelezo baada ya kumsababishia umauti dereva wa pikipiki

Mtoto wa aliyekuwa waziri mkuu wa Kenya na mwenyekiti wa chama cha ODM, Raila Odinga, Fidel Odinga  amefariki Dunia leo alfajiri nyumbani kwake nchini Kenya.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari, Fidel Odinga amefariki akiwa na umri wa miaka 41 akiwa ni mtoto wa kwanza kati ya watoto wanne wa Bwana Raila Odinga.

Chanzo cha kifo hicho bado hakijafahamika na Raila Odinga amethibitisha kifo hicho na kusema kuwa mwanae alikimbizwa hospitalini na mkewe baada ya kuwasili nyumbani majira ya saa 7 usiku wa kuamkia leo na kulalamika kuwa anapata shida katika upumuaji.

Fidel na baba yake Raila walipata chakula cha mchana na kiongozi mmoja hapo jana na baadae jioni marehemu alitoka na marafiki zake ambapo alirejea nyumbani majira ya saa 7 usiku.

Marehemu Fidel Odinga ameacha familia ya mke na mtoto mmoja ambapo inaelezwa kuwa alikuwa ni kijana mwenye ndoto ya kuingia kwenye siasi na kutajwa kama mmoja kati ya wafanyabiashara wakubwa nchini Kenya.

Polisi nchini Kenya wanaendelea kufanya uchunguzi wa chanzo cha kifo cha marehemu.

Msiba huo mkubwa na wakushtukiza katika Taifa utafanyika nyumbani kwa baba yake Raila Odinga.

Viongozi mbalimbali wa vyama nchini humo wameendelea kumiminika kumpa pole  Bwana Raila Odinga kufuatia msiba huo mkubwa wa mtoto wake.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s