FLORA MBASHA AANIKA MAOVU YA MUMEWE, ADAI HAKUWAHI KUMPENDA BALI ALIMUOA KWA AJILI YA KWENDA ULAYA

Flora Mbasha na Emmanuel Mbasha

Pichani ni Flora Mbasha na mumewe kabla ya kutengana

Mwimbaji mahiri wa nyimbo za injili nchini, Flora Mbasha amefunguka kwa mara nyingine tena kuhusiana na sakata la kutengana na mumewe Emmanuel Mbasha kutokana na vituko alivyokuwa akimfanyia ndani ya nyumba.

Akiongea na Uhuru Fm kupitia  kipindi cha Misukosuko ya Maisha, Flora Mbasha amesema amesikitishwa sana na wanawake wenzake ambao wamekuwa wakimsema vibaya kwenye mitandao ya kijamii kuwa anamatatizo na kuwataka watu wasipende kuamini vitu vya kusikia.

imenishangaza kuona kwamba badala ya wanawake ndio wangenisapoti hata mimi mwanamke mwenzao, lakini wanawake ndio wamekuwa wabaya kwelikweli bora hata wanaume.  Yaani ukiingia kwenye mitandao wanaotukana ni wanawake”, alisema Flora.

Aidha Flora amefunguka kwamba mume wake alikuwa akimtamkia mara kwa mara kuwa hakuwahi kumpenda bali  alimuoa kwa ajili ya kwenda ulaya tu huku akimtajia aina tofauti za wanawake awapendao.

Anaongea mwenyewe kwa kinywa chake kwamba mimi nilikuoa kwa ajili ya kwenda Ulaya tu, sasa hivi niishi na wewe kwa ajili ya nini sasa, nikitaka kwenda Ulaya sasa hivi muda wowote naweza nikaenda Ulaya”, alisema Flora.

Kitu kingine ambacho amesema hawezi kukisahau ni pale mumewe alipokuwa akimlazimisha kufanya mapenzi kinyume na maumbile na alipokataa aliambulia kipigo pamoja matusi ambayo yalipelekea mama yake mzazi aache kumtembelea nyumbani kwake.

Kitendo cha kunilazimisha kufanya mapenzi kinyume na maumbile, hicho ni kitu kibaya kabisa kwa sababu najua ni dhambi mbele za Mungu, hicho ndio ambacho kilikuwa kinanipa kipigo kikumbwa kwenye ndoa, kwa sababu kila ninapokataa ni kipigo tuu”, alisema Flora mbasha.

Aliongeza : ”Lakini pia ni matusi ambayo nilikuwa ninayapata, sio mimi tu akianza kutukana anatukana matusi ya nguoni mpaka kwa mama yangu, mimi mama yangu alishaacha kuja nyumbani kwangu kukaa, hata kama akija Dar es salaam kutibiwa anafikia  hotelini, hawezi kuja nyumbani kwangu anaogopa, kwa sababu alishaonywa na Mbasha akae mbali na mimi”.

Mwaka jana wanandoa hao walitawala kwenye vichwa vingi vya habari baada ya Flora kumtuhumu mumewe kumbaka mdogo wake halikadhalika na kwa upande wa Mbasha kudai kuwa mwimbaji huo amekuwa kwenye mahusiano na wanaume wengine.

ANGALIZO : Kwa wale watakaopenda kui-copy hii habari hapa ni ruksa ila msisahau kuandika sehemu mlipoitoa.

Advertisements

4 thoughts on “FLORA MBASHA AANIKA MAOVU YA MUMEWE, ADAI HAKUWAHI KUMPENDA BALI ALIMUOA KWA AJILI YA KWENDA ULAYA

  1. Hata kama ndivyo inaumiza sana,lakini wewe kama mkirsto yaanini kujianika kwenye vyombo vya habari mambo yenu ya ndani? kwanini usiende kwa wachungaji na sio Gwajima maana tayari mumeo anamtuhumu,nenda kwa wazee wakanisa,washenga,wazazi na pia kaa chini na mmeo fungeni na kuomba Mungu atawaonesha njia na ikishindikana mwachane kistaarabu c maneno,tena utaonekana mwanamke ulieokoka na kumfuata kirsto

  2. pole Dada yng frola mungu atakusaidia yataisha ila muombe sana mungu naomba namba yako ili tuwasiliane tupeane mawazo dada yng

  3. Pole sana dadaangu jipemoyo utashinda. Maana shetani anatafuta njia Yakualibu imani yako.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s