DIAMOND KUTUMBUZIA KATIKA UTOAJI WA TUZO ZA WANAMICHEZO BORA AFRIKA

Diamond Platnumz BujuMwanamuziki wa kizazi kipya Bongo, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ anatarajiwa kuburudisha katika sherehe za utoaji Tuzo za wanamichezo bora zinazoandaliwa na shirikisho la mchezo wa soka barani Afrika ‘CAF’, January 08, mwaka huu jijini Lagos nchini nigeria.

Diamond anatarajiwa kuungana na wasanii wengine mahiri barani Afrika walioalikwa kutumbuiza sherehe hizo ambao ni pamoja na Hugh Masekela wa Afrika kusini, Flavour wa Nigeria, Fally Ipupa wa Congo, kikundi cha Pan Africa kutoka Soweto Africa Kusini na P-square wa Nigeria.

Tuzo zinazowaniwa ni mchezaji bora wa Afrika wa mwaka ndani na nje ya bara, Timu bora ya taifa ya mwaka, klabu bora ya mwaka na kocha bora wa mwaka.

Aidha itawaniwa pia Tuzo ya timu bora ya Taifa ya wanawake, mwanasoka bora wa kike, Chipukizi bora, mwamuzi bora na mchezaji bora wa mwaka.

Straika wa Cameroon, Samuel Etoo Fils aliwahi kushinda Tuzo hizi mwaka 2005 na 2010, Didier Drogba wa Ivory Coast alitwaa mwaka 2006 na 2009 huku Frederic Kanoute wa mali mwaka 2007, Adebayor wa Togo mwaka 2008 kabla ya Yaya Toure wa Ivory Coast kutoa mfululizo mwaka 2011,2012 na 2013 lakini pia anatabiriwa kutoa kwa mara nyingine.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s