POLISI WAKAMATA VIJANA 36 WA KUNDI LA PANYA ROAD

Panya Road  Jeshi la Polisi mkoani Dar es salaam linawashikilia vijana 36 wa kundi linalojiita Panya Road kwa tuhuma za kufanya vurugu, kupora mali za watu na kusababisha taharuki katika jiji la Dar es salaam.

Msemaji wa Polisi mratibiu mwandamizi wa polisi, Adivera Bulimba  ameyasema hayo alipozungumza na waandishi wa habari kufafanua taharuki iliyotokea jana jijini Dar es salaam.

Mbali na kuwahakikishia wakazi wa jiji la Dar es salaam kuwa hali iyo haitajitokeza tena amesema jeshi hilo limejipanga vizuri kukabiliana na kikundi chochote kitakachotaka kuleta vurugu na kutishia amani ya nchi.

Amesema kama polisi wamewadhibiti vijana hao mapema tangu wakiwa makaburini baada ya kumzika mwenzao aliyeuwawa na wananchi baada ya kuiba hali ingekuwa mbaya zaidi.

Taharuki iyo ilitokea usiku wa jana baada ya kijana mmoja aliyejulikana kwa jina la Mohammed Ayubu kuuwawa na wananchini Januari Mosi eneo la Tandale kwa mtogole kwa tuhuma za wizi na maziko kufanyika jana na baada ya maziko hayo vijana wenzake walijipanga kufanya fujo ili kulipiza kisasi.

Chanzo : ITV

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s