MTUHUMIWA WA UGAIDI AFARIKI KABLA YA HUKUMU KUSIKILIZWA

Abu Anas Al-Libi

Abu Anas Al-Libi

Mtu mmoja anayesadikiwa kuwa mfuasi wa kikundi cha Al Qaedar anayetuhumiwa kuzishambulia ofisa za ubalozi wa Marekani za Dar es salaam na Nairobi mwaka 1998 amefariki Dunia jijini New York siku chache kabla ya kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma hizo.

Mke wa mtuhumiwa uyo na wakili wake wamesema Libi  amefariki Dunia kwa saratani ya ini katika hospitali moja jijini New York.

Bwana Libi mwenye umri wa miaka 50 alikamatwa mjini Tripoli nchini Libya Oktoba 2013 kufuatia shambulio lililofanywa na makachero wa Marekani katika jengo moja mjini humo.

Abdullah al-Raghie (left), and , the son and brother respectively, of al-Qaeda suspect Abu Anas al-Libi speak to the press in Nofleine, near the Libyan capital Tripoli (file)

Mtoto wa marehemu, Abdullah Al-Raghie(Wa Kwanza) katika picha na kaka wa marehemu bwana Nabih al-Raghie wakizungumza na vyombo vya habari jijini Tripoli nchini Libya

Mtuhumiwa uyo alitarajiwa kufikishwa mahakamani Januari 12 mwaka huu kujibu shitaka la kushiriki katika mashambulio hayo katika miji ya Nairobi na Dar es salaam yaliyosababisha vifo vya zaidi  ya watu 220.

Bwana Abu Anas Al-Libi ambaye jina lake halisi ni Nazih Abdul-Hamed Al-Ruqai alitoa utetezi wa kukanusha kuhusika kwa namna yoyote na tuhuma za Ugaidi zilizotajwa dhidi yake.

Wakati alipokamatwa mwaka 2013 alikuwa kwenye orodha ya shirika la upelelezi la Marekani akiwa miongoni mwa watu wanaotafutwa kwa karibu muongo mmoja ambapo dhamana ya dola milioni 5 ilikuwepo kwa yeyote angefanikisha kupatikana kwake.

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s