MATEMBEZI YA WAFUASI WA CHADEMA WALIOTOKA SHINYANGA MPAKA DAR KWA MIGUU YAISHIA POLISI SIYO IKULU

Wazalendo wa ChademaVijana watatu wakiwa na wafuasi wao walioandamana kutoka Nzega kuja Dar es salaam kwa madai ya kuja Ikulu kumuona Rais na kumlalamikia juu ya mambo mbalimbali yanayoikabili Taifa wamekamatwa na kufikishwa kituo cha Magomeni kwa mahojiano zaidi.

Akithibitisha kukamatwa kwa vijana hao, Kamanda wa polisi mkoa wa kipolisi Kinondoni, Camilius Wambura amesema mji wa Dar es salaam unaendeshwa kwa sheria na taratibu maalum na hivyo ni vyema watu wafuate sheria na taratibu katika utekelezaji wa madai mbalimbali wanayotaka kuwasilisha kwa serikali.

Mwaka 2015 majira kama ya saa 3 asubuhi tulipata taarifa kwamba kuna vijana watatu wakiwa wameandamana na watu wengine ambao ni zaidi ya kumi, kumi na tano kwenda ishirini kuanzia maeneo ya Kibaha na kwenda Ikulu kumuona muheshimiwa Rais kwa mambo yao mbalimbali ambayo walikuwa wanasema wanahitaji kumuona na kumfikishia ujumbe wao”, alisema Wambura.

Lakini ilionekana watu hao kuwa ni vyema wakakutana na mkuu wa  wilaya na walikutana nae wakaongea nae na akapokea ujumbe wao na aliahidi kuufikisha kwa mheshimiwa Rais kwa taratibu za kiserikali na baada ya hapo walielekezwa kwamba basi safari yao ya kuelekea Ikulu ilikuwa imeishia hapo ujumbe wao ungefika kwa njia ya kwake”.

Kamanda Wambura amesema serikali imewaachia kwa dhamana vijana sita ambapo watatu kati yao ndio waliotoka Mwanza kwa kutembea kwa miguu na Polisi inaendelea na uchunguzi zaidi huku taratibu nyingine za kisheria zikizingatiwa.

Chadema Wazalendo Vijana Wazalendo  wazalendo Wazalendo1

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s