EPL : MATOKEO YA MECHI ZILIZOCHEZWA JANUARI MOSI MWAKA MPYA

Ligi kuu ya England imeendelea kutimua vumbi kwa mwaka mpya wa 2015 baada ya michezo takribani 10 kupigwa kwenye madimba mbalimbali barani Ulaya Jan 01.

Harry KaneSTOKE CITY 1 – 1 MANCHESTER UNITED

Mashetani wekundi klabu ya Manchester United ikiwa ugenini ililazimishwa sare ya 1 – 1 na Stoke City katika mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Britannia.

Stoke ndio waliokuwa wa kwanza kuzifumania nyavu za United kupitia mchezaji wake Ryan Shawcross kabla ya kusawazishwa na Radamel Falcao dk ya 26′ na mchezo kumalizika kwa sare ya moja moja.

TOTTENHAM HOTSPURS 5 – 3 CHELSEA

Mchezo mwingine uliokuwa na upinzani mkali ni ule uliowakutanisha Chelsea waliokuwa wageni wa Tottenham Hotspurs ambapo mpaka kipenga cha mwisho kinapigwa The Blues walijikuta wakilazwa kwa jumla ya magoli matano kwa matatu.

Licha ya Chelsea kuwa wa kwanza kuliona lango la Spurs haikuweza kuwasaidia  badala yake walijikuta wakipewa mvua ya magoli kutoka kwa Harry Kane aliyefunga Hat-Trick(Mabao 3), Danny Rose, Andros Townsend kwa mkwaju wa penalti na Nacer Chadli wakati kwa chelsea mabao yao yakifungwa na Diego Costa aliyeifungia goli la kuongoza, Eden Hazard na John Terry.

MANCHESTER CITY 3 – 2 SUNDERLAND

Manchester City waliikaribisha nyumbani klabu ya Sunderland  kwa kuipa kipigo cha bao tatu kwa mbili katika mtanange uliochezwa kwenye dimba la Etihad.

Mabao ya City yaliwekwa wavuni na Kiungo wa Ivory Coast Yaya Toure, Stevan Jovetic na Frank Lampard huku kwa upande wa Sunderland yakifungwa na Jack Rodwell na Adam Johnson kwa mkwaju wa penalti.

LIVERPOOL 2 – 2 LEICESTER CITY

Majogoo wa jiji la London, Liverpool Fc walijikuta wakikabwa koo kwa kulazimishwa sare ya bao 2 – 2 na Leicester City katika mchezo  uliochezwa kwenye uwanja wa Anifield.

Kapteni wa Liverpool Steven Gerrard aliipatia timu yake mabao mawili yaliyopatikana kwa njia ya mikwaju ya penalti mnamo dakika ya 21′ na 40′ kabla ya David Nugent na Jeffrey Schlupp kusawazishwa  na kujikuta wakigawana alama moja.

SOUTHAMPTON 2  –  0  ARSENAL

Washika mtutu wa jiji la London, Arsenal walijikuta wakikubali kipigo cha bao mbili kwa nunge nyumbani kwa Southampton katika mchezo uliopigwa kwenye dimba la St Mary’s.

Mabao ya Southampton yaliwekwa kimyani na Sadio Mane pamoja na Dusan Tadic yaliowawezesha kutwaa alamu 3 muhimu ambazo zimewaweka kwenye nafasi ya nne katika msimamo wa ligi kuu ikiwa na jumla ya alama 36 nyuma ya United.

Unaweza ukatazama msimamo mzima wa ligi kuu ya England hapo chini

epl

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s