MAN CITY YAMUONGEZEA MKATABA FRANK LAMPARD HADI MWISHO WA MSIMU

Frank Lampard

Hatimaye Klabu ya Manchester City imemuongezea mkataba kiungo mkongwe Frank Lampard hadi mwisho wa msimu wa ligi kuu.

Lampard mwenye miaka 36 amemaliza mkataba wake na klabu ya New York City ya Marekani usiku wa kuamikia leo kwa maana iyo atabakia Etihad hadi mwisho wa msimu na atakosa mechi za mwanzo za ligi kuu ya Marekani ‘Major League’ au MLS.

Klabu ya New York City ilimsaini Lampard mara baada ya kuachwa na Chelsea ya England Juni mwaka jana na klabu ya Manchester City kumuomba kurejea ili acheze kwa mkopo kwa kuwa ligi ya marekani inaanza March mwaka huu.

Kuongezewa mkataba kwa Lampard kumekuwa ni faraja kubwa kwa kocha Emmanuel Pellegrini kwa kuwa atakuwa mbadala wa kiungo Yaya Toure anayejiunga na timu yake ya Taifa Ivory Coast kuanzia January, 05 katika fainali za Afrika nchini Guinnea ya ‘GuinneEquator.

Lampard amekishwa ichezea Manchester City mechi 17 akiwa ameweka wavuni mabao 6 huku akitajwa kuwepo katika kikosi cha leo kitakachovaana na timu ya Sunderland kwenye uwanja wa Etihad.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s