WASANII WAZUNGUMZIA SHOO YA PRINCE DULLY SYKES YA MIAKA 15 KATIKA BONGO FLAVA

Dully Sykes - Larrybway91 BlogLegendary wa Bongo Flava na mmiliki wa studio ya 4.12, Prince Dully Sykes au Bwege la Kizaramo kama anavyojiita ameweka historia ya aina yake kwenye kiota cha burudani hapa Bongo ‘Escape One’ usiku wa Desemba 30 wakati alipokuwa akijipongeza kwa  kutimiza miaka 15 kwenye gemu la muziki wa Bongo Flava.

Shoo iyo iliyopewa jina la Miaka 15 ya Bongo Flava ilisindikizwa na wasanii kibao wakiwemo waliowahi kufanya kazi pamoja na Dully enzi hizo na wale aliowatambulisha katika gemu akiwemo Mwana FA, Ally Kiba, Bushoke,Christian Bella, Banana Zoro, Queen Darleen, Makomando, Linah, Madee, Chege, Temba na wengine wengi ambao baadhi yao waliweza kuizungumzia shoo ya mwanamuziki uyo akiwemo Q-Chief aliyeshindwa kuvumilia na kujikuta akimwaga machozi.

I’m just happy,… i’m happy for Dully Sykes…i’m happy kwamba watu wamekuja wengi wanakumbuka kwa kuthamini vitu vizuri ambavyo amefanya..to me it is always nice..it is always a great things..it is always a great stuff..kwaiyo nampongeza Dully Sykes ..nimelia ati kuona watu wanampenda kiasi gani..sijalia kuhusu mimi wala nini..mimi always nina hisia kwa wenzangu..i don’t know i love a thing”, alisema Q Chief

Nilikuwepo kwenye shoo ya Dully….nilikuwepo aaah!!miaka 15 si midogo unajua…so Dully amekamata watu wa rika zote toka anaanza muziki wake.. kwaiyo ame-maintain fresh tu..tunaona wanamuziki wengi wa sasa hivi wanafanya miaka miiwli mitatu mbele wanapotea”, alisema Madee

Baaab kubwa..yaaani baab kubwa..kwa sababu Dully ni msanii ambaye kwa watu wanamjua before utamuheshimu Dully kitu anachofanya…amekaa miaka yote Dully sijasikia kapotea, Dully akitoka anatoka, Dully akitoka anatoka ..Dully ndio msanii ambaye anaongoza kwa kuwa na hit songs nyingi Tanzania kwa kweli yaani..kwaiyo Big time kwa Dully..mimi nina miaka kama 13 hivi ..Mungu amsaidie, amuendelezee kipaji, amuendelezee kuwa creative, kaanzisha Bongo Flava, Bongo Fleva wameimba watu wengi lakini yeye amekuwa chachu ya Bongo Flava na mpaka leo bado anafanya kwaiyo mimi nam-respect sana Dully Sykes”, alifunguka Chege Chigunda

we got History,…it is a great things to celebrate,, kwa sababu yaani hii inaonyesha kwamba yeye mwenyewe ni kama artist ame-appreciate alipotokea mpaka alipofikia na inaonekana kabisa siku zinavyozidi kwenda atafikia mbali mbali zaidi,..this is a great artist..great person like a human like i said”, alisema mmiliki wa  B-Band Banana Zorro

tumekuja ku-support braza,..inaonyesha kabisa ana watu pia wachapakazi ambao wanamuheshimu..unajua tunaheshimiana katika life kwaiyo watu kama sisi hivi..umeona wakina banana zorro… hawa ni watu wakongwe katika hii gemu hii..umeona kabisa akigusa tu lazima watu walalamike..sisi tukigusa mashabiki wanaitikia..tumeacha makazi zetu tumekuja hapa ku-support bila kulipwa chochote..tumejitolea..unajua kuna wasanii wengi wanakata tamaa..lakini jamaa(Akimaanisha Dully Sykes) anajua kwamba yeye ni supastaa mpaka kesho..ni mbishi sana alafu mimi namtaka aendelee hivyo hivyo ..unaona kuna wasanii ambao alianza miaka moja nao hawafanyi tena music lakini yeye mpaka leo bado anabisha..aendelee hivyo hivyo..mimi namtakia kila la kheri..aendelee mpaka siku ambayo atastafu..tutaendelea tena kum-support mpaka siku akisema anastafu lakini wakina Koffi mpaka leo hawajastafu..wewe utastafu vipi??alifunguka King of the best melodies Christian Bella

Dully Sykes pia alipata nafasi ya kuzungumzia juu ya siku yake iyo muhimu na kile anachojivunia kwa miaka yote iyo 15 ya kuweza kudumu katika gemu la muziki wa Bongo Flava.

Najivunia kukumbukwa kama msanii ambaye amekuwa muasisi wa huu muziki..najivunia kwa hilo..kuna wengi ambao walikufa bila kukumbukwa lakini mimi kabla sijafa nimekumbukwa…najivunia..challenge ni nyingi sana lakini nimezishinda zote..kuna wasanii walikuja wakaimba wakawa juu, wakapata hela zaidi ya mimi lakini bado mimi na wao mimi nafanya vizuri…sikutegemea kumuona Chege, sikutegemea kumuona madee, Dogo Janja na pia sikutegemea kumuona Ally Kiba katika hii shoo yangu..kwiayo nafurahi nimewaona pia nawashikaji zangu ambao nimecheza nao zamani ambao nimeanza nao mbali..nimewaona nimefurahi pia..unajua shoo nyingi za wasanii huwa zinasuswa na wasanii, lakini mimi nimefurahia kuona wasanii ambao..kuna wasanii ambao ni wengi nimeanza nao siku nyingi walishindwa kuja hapa kwa sababu hata wasingeweza kulipa”, alisema Dully Sykes

Aliendelea kwa kufunguka,”leo nimemuona MwanaFA ameperform kwenye stage yangu, Banana Zorro..nimefurahi sana..mimi imenipa hamasa wanasema..imenizidishia mapenzi kwao..pia nafurahi Q Chief amekuja,…uwepo wa Q Chief na Bushoke pia..uwepo wao mimi nimefurahi kwa sababu sijategemea wale..kuna wasanii ambao nilitakiwa yaani wadogo zangu kuna vijana ambao nimewataja katika posters lakini hawajatokea..imenisikitisha sana..wasanii ambao mimi nimewalea..wamekula jasho langu..sisemei kwa ubaya kwa sababu sizoeagi  kusema ivyo..msanii ambaye amejitolea ni Diamond peke yake katika wale wasanii ambao nimewasaidia na Ally Kiba kwa sababu ndio alikuja hapa na wengine vijana ambao wameimba akina Makomando, Queen Darlin ndio wamejitolea..kwa sababu Diamond japo hayupo lakini ameandika kwenye Instagram kwa masikitiko kabisa kwamba alitakiwa awepo lakini anasikitika kuikosa shoo kubwa kama hii na alitakiwa yeye awepo

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s