MTUHUMIWA WA DAWA ZA KULEVYA ATWANGWA RISASI NA POLISI MAHAKAMA YA KISUTU JIJINI DAR

Mtuhumiwa wa Dawa za Kulevya apigwa risasi

Pichani ni mtuhumiwa wa Dawa za kulevya akiwa amening’inia kwenye uzio wa mahakama ya Kisutu asubuhi ya leo baada ya kuuwawa kwa kupigwa risasi na Polisi wakati akijaribu kutoroka

Polisi jijini Dar es salaam wamemuua kwa kumpiga risasi mahabusu mmoja kutoka gereza la keko aliyetoroka akiwa chini ya ulinzi katika mahakama ya hakimu mkazi kisutu.

Mahabusu uyo Abdul Koroma Raia wa Sierra Leone aliyekuwa akikabiliwa na tuhuma za kukutwa na dawa za kulevya ameuwawa alipokuwa akikimbia baada ya kufunguliwa kutoka kwenye chumba cha mahabusi cha mahakama iyo ili aingie kwenye gari kumrejesha gerezani.

Walioshuhudia tukio hilo wamesema wakati mahabusu uyo alipoanza kukimbia askari wa magereza alifyatua risasi moja hewani ili kumuonya asikimbie lakini hakufanya ivyo ndipo akampiga mkononi lakini aliendelea kukimbia na kuruka uzio wa lango la mahakama hadi nje ndipo alipopigwa risasi nyingine kichwani iliyomsababishia kifo chake.

Kamanda wa Polisi kanda maalum ya Dar es salaam Suleiman Kova amedhibitisha tukio hilo na kusema kuwa mapolisi wanaendelea na uchunguzi ili kubaini chanzo chake.

Mtuhumiwa wa Dawa za Kulevya Kisutu

Picha nyingine ikimuonyesha mtuhumiwa uyo akiwa amening’inia huku akichuruzika damu.

mtuhumiwa wa dawa za kulevya

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s