FILAMU YA ”THE INTERVIEW” YAVUNJA REKODI YA MAUZO

The Interview.jpg1Kampuni ya Sony imesema kuwa filamu ya ”The Interview”  imenunuliwa mtandaoni zaidi ya mara milioni 2 na kuzalisha zaidi ya dola milioni 15 katika siku nne za kwanza. 

Aidha kampuni iyo imesema kuwa filamu iyo inayopatika katika mitandao ya Google, Youtube, Microsoft Xbox Video na katika tovuti yenye muonekano wa HD hukodishwa kwa muda wa saa 48 kwa dola 5.99 na kuuzwa kwa dola 14.99. 

Takwimu hizi zinaifanya filamu hii iliyochezwa na Seth Rogen pamoja na James Franco kuvunja rekodi katika kampuni ya Sony kwa mauzo na kuangaliwa zaidi kupitia mitandao kwa muda wa siku chache zaidi tangu kutolewa rasmi.

Mapema kampuni ya Sony Pictures ilihairisha mpango wake wa kuiachia filamu iyo katika siku ya  Christmas baada ya kompyuta za kampuni iyo kudaiwa kuingiliwa na wadukuzi huku Korea ya kaskazini ikihusishwa katika udukuzi huo.  Itazame Trailer yake hapo chini

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s