Mchekeshaji maarufu ambaye pia ni muigizaji filamu Marekani, Chris Rock ametoa uamuzi wa kutengana na mkewe aliyedumu nae kwa muda wa takribani miaka 20.
Mke wa mchekeshaji huyo aitwaye Malaak Compton alitoa taarifa Jumapili kwa watu za kutengana na staa uyo akinukuliwa akisema,”Baada ya kutafakari sana na miaka 19 ya ndoa, Chris na mimi tumeamua kutengana”.
Aliongeza kuwa, ”wakati nikitambua kwamba haya ni mabadiliko makubwa, watoto wangu watabaki katikati ya maisha yangu na ustawi wao ni kipaumbele juu yangu”.
Aidha mwanasheria wa Chris amethibitisha kufunguliwa kwa jalada la talaka na mteja wake ambaye mwaka 2006 aliwahi kuripotiwa kutaka kutalikiana na mkewe uyo kabla ya kuamua kukaa chini na kuyamaliza.
Chris mwenye umri wa miaka 49 alifunga ndoa na mkewe mwaka 1996 na kufanikiwa kupata watoto wa kike wawili ambao ni Lola Simone mwenye miaka 12 na Zahra Savannah miaka 10.