Chris Brown na mpenzi wake karrueche wamepigia mstari ule msemo usemao, ”True LoveS Never Dies”, baada ya kuonekana tena wakiwa pamoja na mbwa wao eneo la Beverly Hills nchini Marekani.
Awali wapenzi hao walionekana kwa mara ya kwanza wakitoka kwenye klabu moja ya usiku mjini Los Angels tangu waliporipotiwa kumwagana na kutoleana maneno ya kashfa mitandaoni kwa kile kilichotajwa kuwa ni kukosekana kwa uaminifu katika penzi lao.
Inaelezwa kurudiana kwao kunakuja kufuatia Chris brown kumnunulia pete mbili za almasi Karrueche ikiwa ni sehemu ya kuomba msamaha na zawadi ya Christmas.
”Christmas Pup’. Could it have been another gift from Breezy? Probably”, aliandika Karrueche kwenye ukurasa wake wa Twitter siku ya Christmas na ku-post picha ya mbwa uyo.