IDRIS AZUNGUMZIA MIPANGO YAKE YA MWAKA 2015

Idris SultanMshindi wa shindano la Big Brother Hotshots, Idris Sultan au unaweza kumuita Tajiri mtoto amefunguka mengi juu ya mikakati na mipango anayotarajia kuifanya mwaka 2015 kupitia dola 300,000 alizopata kama  zawadi kwenye shindano hilo.

Akiongea kwenye kipindi cha Tuambie Tz kinachorushwa hewani na kituo cha Choice Fm, Idris alisema anampango wa kuitunisha akaunti yake mara saba na kuongeza kwamba mipango yote anayoipanga sasa hivi haihusiana na hela aliyoipata.

Napanga ku-maximize  akaunti yangu mara saba, plan zote ambazo nazipanga kuzifanya sasa hivi hazihusiani na ile niliyopata mimi, zinahusiana na ile platform ambayo mimi nimeipata Big Brother, alisema Idris.  ”Kwaiyo nataka nifanye mikakati mingi huku nje kwaiyo mpaka nikiangilia mpaka mwisho wa mwaka nitakuwa na akaunti kubwa zaidi ambayo itanisaidia sasa kufanya vitu vikubwa zaidi”.

Idris mwenye umri wa miaka 21 amezungumzia pia mipango mingine ikiwemo suala zima la kuwarudishia shukrani waafrika kwa kusaidia jamii, kufanya shows,  Tv Shows, live shows na suala zima la kurudi shule.

Napanga kwenda kama nchi tatu hivi kwenda kufanya kozi tofauti, nataka niende Italy, nataka niende London, nataka niende pia Marekani. sasa hivi nahisi hata Hollywood nataka niende”, alifunguka Idris.

 

 

 

 

 

 

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s