AZAM FC NA YANGA ZATOKA SARE YA MBILI MBILI

Azam FcLigi kuu ya kabumbu Tanzania bara imechanja mbuga hii leo(Dec.28) kwa michezo kadhaa kuchezwa ukiwemo wa mafahali wawili  Azam Fc dhidi ya mahasimu wao Yanga katika mtanange uliopigwa uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Azam Fc ndio ilitangulia kupata bao lake la kwanza katika dakika ya 5 kupitia kwa mchezaji wake Sure Boy, dakika moja baadae Yanga walisawazisha kupitia mchezaji wake Hamis Tambwe baada ya kupata mpira kutoka kwa Saimon Msuva.

Baada ya mapumziko timu zote zilishambuliana zamu kwa zamu, Yanga walifanikiwa kuongeza goli la pili kupitia Saimon Msuva kabla ya kusawazishwa na John Bocco ‘Adebayor’ mara baada ya kuingia uwanjani.

Huko Mbeya timu ya Mbeya City imeifunga Ndanda Fc bao moja kwa bila, Polisi Morogoro ikiifunga Mgambo bao moja kwa bila.

Wakati pambano la Stand United dhidi ya Mtibwa likihitimika kwa sare ya bao moja kwa moja  katika mchezo uliochezwa mji kasoro bahari ‘Morogoro’.

 

 

Advertisements

One thought on “AZAM FC NA YANGA ZATOKA SARE YA MBILI MBILI

  1. Azam hawana kitu hio sare wamebahatisha tu, ngoja itakapo fika mwakan watajua kuwa hii ni yanga au co yanga

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s