PATCHO MWAMBA : SIJAFUMANIWA NA MKE WA MTU NI ALEJI YA MACHO TU!

Pichani Patcho mwamba Kabla na baada ya kupata Aleji

Pichani ni Patcho mwamba Kabla na baada ya kupata kasumba hiyo

Mwanamuziki wa Bendi ya wazee wa Ngwasuma Fm Academia na mwigizaji wa Bongo Movie, Patcho Mwamba amekanusha vikali habari zilizozagaa kwenye mitandao na media mbalimbali akidaiwa kuchezea kichapo baada ya kufumaniwa na mke wa mtu eneo la Kinondoni Jijini Dar es salaam.

Kwa mujibu wa tovuti ya Global Publishers ilimnukuu Patcho akisema picha iliyozagaa mitandaoni ikimuonyesha ameumuka usoni ni yeye mwenyewe aliamua kuisambaza baada ya kupata aleji ya macho kutokana na kunywa pombe.

Unajua nina aleji na pombe pamoja na vumbi, nikitumia tu pombe lazima macho yangu yavimbe” alisema Patcho na kuongeza, ”juzi nilikunywa Windhoek mbili na usiku hali yangu ikabadilika na macho kuvimba, baada ya tukio hilo niliamua kujipiga picha na kuipost katika mtandao wa Instagram na hapo ndipo balaa likazuka”.

 

Advertisements

One thought on “PATCHO MWAMBA : SIJAFUMANIWA NA MKE WA MTU NI ALEJI YA MACHO TU!

  1. Patcho achana na Pombe rudi kundini, nenda Efatha kama mama wako, Tazama Mke wako na watoto wako wameokoka , na tunasali nao Efatha kwa baba yetu wa kiroho mwingira

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s