MAUAJI TENA!!! KIJANA MWINGINE MWEUSI AUWAWA KWA KUPIGWA RISASI NA AFISA POLISI MJINI MISSOURI

Missouri

waandamanaji wakifanya yao eneo la kituo cha gesi yalipotokea mauaji

Uhasama baina ya mapolisi na watu weusi umeonekana kuendelea kushika kasi  baada ya kijana mwingine mweusi kuripotiwa kuuwawa kwa kupigwa risasi na afisa polisi usiku wa Jumanne(Dec.23) kwenye kituo kimoja cha gesi kilichopo eneo la Berkeley, Missouri nchini Marekani.

Vyombo vya habari vimemnukuu msemaji wa Idara ya polisi  wa St.Louis, Sajenti Brian Schellman katika taarifa yake akisema afisa huyo wa polisi alikuwa katika kituo cha gesi  kilichopo katika kitongoji cha St.Lous na alipogundua akifuatwa na watu wawili, mmoja wao akidaiwa kuwa na silaha mkononi , afisa aliwafyatulia risasi na kumuua kijana uyo hali iliyopelekea mwenzake kutimua mbio.

Wakati polisi wakikataa kutaja jina la muhanga wa tukio hilo, mwanamke ambaye alitambuliwa na vyombo vya habari kwa jina la Toni Martin alikiambia kituo cha NBC kuwa marehemu  ni  mtoto wake wa kiume anayeitwa Antonio Martin mwenye umri wa miaka 18  na kudai  mwanae alitoka kwenda kumtembelea mpenzi wake.

”Aliondoka nyumbani kwenda kumuona mpenzi wake. Labda alianza kukimbia na wao wakampiga risasi”, alisema Toni huku akitokwa na machozi na kuongeza kwamba hafikirii kama mtoto wake alibeba silaha.

Toni martin aliongezea kwa kusema mpenzi wa mtoto wake ndiye aliyemjulisha kuhusu shambulio la risasi na kumpeleka hadi eneo la tukio na kukuta maandamano makubwa ya Raia wakipinga vikali mauaji hayo.

Hivi karibuni kumekuwepo na  mfululizo wa matukio ya vifo vya watu weusi kuuwawa kwa kupigwa risasi na maafisa polisi wazungu nchini marekani hali inayopelekea kuchochea vitendo vya kibaguzi na uadui mkubwa baina ya matabaka hayo mawili.

Miongoni mwa vifo vya watu weusi vilivyowahi kuvuta hisia za watu wengi nchini humo ni pamoja na kifo cha Trayvon Martin, Eric Garner, Mike Brown na kijana Ismaaiyl Brinsley aliyejitoa muhanga  kwa kuwauwa kwa risasi maafisa wawili wa polisi na kisha mwenyewe kujimaliza mjini Brooklyn.

Mama mzazi wa marehemu Antonio, Toni Martin akilia kwa uchungu eneo la tukio

Mama mzazi wa marehemu Antonio, Toni Martin akilia kwa uchungu eneo la tukio

Antonio Martin

Baadhi ya waandamanaji wakiwa chini ya ulinzi

Antonio Mauaji

Waandamanaji wanaopinga mauaji ya Antonio wakijibishana na polisi

Antonio1

Uharibifu uliofanywa na waandamanji wa Antonio

Antonia martin

Waandamanaji na polisi wakiwa wamezingira kituo cha gesi eneo yalipotokea mauaji

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s