KIJANA ALIYEWAUA MAAFISA WA POLISI NEW YORK ALIDHAMIRIA

Kijana  'Ismaaiyl Brinsley' katika pozi enzi za uhai wake

Ismaaiyl Brinsley enzi za uhai wake

Polisi mjini New York nchini marekani wanasema kuwa kijana aliyewaua maafisa wawili wa polisi kwa kuwapiga risasi imebainika kuwa kabla ya kufanya shambulio hilo alisikika akiuambia umma waangalie anachokifanya.

Kijana huyo Ismaaiyl Brinsley mwenye umri wa miaka 28 anahistoria ya kufanya uhalifu na matatizo ya akili huku mkesha wa kuwasha mishumaa  ukifanyika jijini humo ikiwa ni katika kuwaenzi maafisa hao wawili wa Polisi ambao ni Rafael Ramos na Wenjian Liu.

Brinsley aliwapiga risasi polisi hao wakiwa kwenye gari doria huko Brooklyn Jumamosi (Dec.20) kabla ya kukimbilia karibu na kituo cha Treni na baadae kujiua.

Mkuu wa upelelezi Robert boyce amesema kuwa Brinsley siku zote alikuwa ni mtu mwenye vurugu na aliandika katika mtandao wa Instagram kuwa atawauwa maafisa wa polisi kwa lengo la kulipiza kisasi  baada ya vijana wawili weusi Eric Gardner na Mike Brown kupoteza maisha baada ya kukamatwa na polisi.

Rafael Ramos

Afisa Rafael Ramos akipewa msaada wa huduma ya kwanza  baada ya kupigwa  risasi

p2

Pichani ni maafisa wa polisi waliouwawa na Brinsley,  Rafael Ramos(wa kwanza kulia) na Wenjian Liu

 

Pichani ni eneo lilipotokea tukio la mauaji ya maafisa hao

 Eneo yalipotokea mauaji ya maafisa hao wa polisi kwenye makutano ya barabara  ya Myrtle na Tompkins

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s