ESSEBSI ASHINDA UCHAGUZI HURU WA KWANZA WA URAIS TUNISIA

Pichani ni Rais mpya wa Tunisia Beji Caid Essebsi

Pichani ni Rais mpya wa Tunisia Beji Caid Essebsi

Mwanasiasa mkongwe wa Tunisia ‘Beji Caid Essebsi’ ameshinda uchaguzi huru wa kwanza wa urais kuwahi kufanyika nchini humo kupitia tiketi ya chama chake cha Nidaa Tounes tangu vuguvugu la mataifa ya kiarabu kumuondoa dikteta Zine El-Abidine Ben Ali mwaka 2011.

kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa Jumatatu(Dec.22)  na mamlaka ya uchaguzi, Essebsi Mwenye umri wa miaka 88, aliibuka mshindi dhidi ya mpinzani wake Moncef Marzouki kwa asilimia 55.68 ya kura kati ya asilimia 44.32 katika uchaguzi uliomalizika  Jumapili(Dec.21) mara baada ya serikali ya mpito nchini humo kuimarisha Demokrasia kwa kipindi cha miaka 4 iliyopita.

Wagombea wote walitakiwa wawe watulivu baada ya maandamano yaliyozuka katika miji kadhaa ya kusini  juu ya kurudi kwa vikosi vya ulinzi vya zamani.

Ushindi huo unaonekana kama kilele cha mageuzi ya kisiasa kwa kuwa nchi hiyo imepitia machafuko kwa takribani miaka 4 iliyopita.

”Nitakuwa Rais kwa ajili ya wananchi wote wa Tunisia’‘, alisema Essebsi katika hotuba fupi aliyokuwa akiitoa kwenye televisheni ya serikali.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s