YANGA YAMTAMBULISHA RASMI KOCHA HANS VAN PLUJIM

Hans Van Pluijm

Pichani ni kocha mpya wa Yanga ‘Hans Van Pluijm’ akisalimiana na mashabiki wa yanga

Inaitwa kata mti panda mti, Kocha mholanzi ‘Hans Van Plujim’ ambaye amerejea kuinoa Yanga kwa mara ya pili baada ya kuisaidia timu hiyo kushika nafasi ya pili msimu uliopita, anachukua mikoba ya kocha mbrazil ‘Marcio Maximo‘ ambaye ametupiwa virago baada ya kufungwa na Simba mabao mawili kwa bila katika mchezo wa nani mtani jembe? uliochezwa Dec.13 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Kocha huyo ambaye aliondoka Yanga baada ya kupata timu nchini Saudi Arabia , amesaini mkataba wa mwaka mmoja na nusu kukinoa kikosi cha Yanga huku akiweka wazi kujitaidi kuifanya Yanga kucheza soka la kuvutia na kuwafanya mashabiki kufurahia mchezo wa mpira wa miguu endapo atapata sapoti ya kutosha kutoka kwa wachezaji, uongozi  na mashabiki .

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s