RAIS KIKWETE AMWAJIBISHA WAZIRI TIBAIJUKA KUFUATIA SAKATA LA ESCROW

Rais KikweteRais Jakaya Mrisho Kikwete ametengua uteuzi wa Waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi Prof.Anna Tibaijuka kutokana na makosa ya ukiukwaji wa maadili ya utumishi ya Umma hasa namna alivyopokea fedha za malipo ya Escrow huku akimweka kiporo Waziri wa Nishati na Madini mheshimiwa Sospeter Muhongo.

Rais Kikwete ameyasema hayo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na wazee wa jiji hili ambapo amesema Serikali haina upungufu wa dhamira  kwa yeyote mwenye utekelezaji wa maazimio ya Bunge na kwa yale yanayohusu utekelezwaji yatatekelezwa na yale yanayozungumzika yatazungumzwa.

Kupokea fedha kutoka V.I.P Engineering & marketing, tumekaa nae na kuzungumza nae na kamati ya maadili imeendelea nae lakini mazungumzo yetu sana yalikuwa pesa hizi ni za nini, amezipata vipi, kwa ajili gani…ameeleza ni pesa kwa ajili ya shule..unaendesha shule..maswali makubwa na maelezo yametolewa, bodi imeeleza, Mzee Rupia na kijana ameeleza ila maswali makubwa ambayo yametia shaka sana na kuleta mjadala mkubwa ni kwanini pesa hizi hazikwenda moja kwa moja huko shule??? alisema Rais Kikwete.

Kuhusu suala la kumwajibisha waziri Sospeter Muongo, Rais Kikwete ameagiza uchunguzi ufanywe na bado hajapata majibu ila ndani ya siku mbili hizi atafanya maamuzi baada ya kujiridhisha ili uamuzi atakaoutoa usiwe wa kumuonea wowote.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s