LIVERPOOL YATOKA SARE YA 2 – 2 NA ARSENAL

Coutinho

Kiungo mkabaji wa Brazil, Coutinho akishangilia baada ya kutupia wavuni bao la kuongoza kwa timu yake ya Liverpool dhidi ya Arsenal

Majogoo wa jiji la London ‘Liverpool’ wameshindwa kufurukuta kwenye uwanja wao wa nyumbani ‘Anfield’ baada ya kutoka  sare ya goli 2 – 2 na klabu ya Arsenal.

Kiungo mkabaji wa Liverpool, Philippe Coutinho aliweza kuipatia timu yake bao la kuongoza,  kabla ya Arsenal kusawazisha na kuongeza kupitia  wachezaji wake mathieu Debuchy mnamo dakika ya 45′ na Oliver Giroud, hata hivyo mambo hayakwenda kama walivyotarajia baada ya beki Martin Skrtel kusawazisha dakika za lala salama.

Mtanange mwingine wa ligi kuu ya England uliopigwa Dec.21, ulikuwa ni kati ya Newcastle waliowakaribisha Sunderland dimbani kwao na kujikuta wakipewa dozi ya bao 1 kwa nunge, goli likifungwa na Adam Johnson.

Kwa matokeo hayo yanaifanya Liverpool ikamate nafasi ya 10 chini ya Newcastle  kwenye msimamo wa ligi kuu ikiwa na alama 22 wakati kwa upande wa Arsena ikishikilia nafasi ya 6 nyuma ya Southampton ikiwa na alama 27 mkononi.

Kiungo mkabaji wa Arsenal 'Mathieu Debuchy' akishangilia baada ya kusawazisha goli la kwanza dhidi ya Liverpool

Mchezaji wa Arsenal ‘Mathieu Debuchy’ akishangilia baada ya kusawazisha goli la kwanza dhidi ya Liverpool

 

Mchezaji wa Arsenal, Oliver Giroud akishangilia sambamba na Welbeck baada ya kuongeza bao la pili kwa Liverpool

 

mashabiki

Mashabiki wa Liverpool wakifuatilia kwa makini mtanange

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s