BONDIA MUHAMMAD ALI ASUMBULIWA NA HOMA YA MAPAFU

Muhammad AliAliyekuwa bingwa mara tatu wa uzito wa juu Duniani, bondia Muhammad Ali amepata nafuu baada ya kupatwa na shambulio la homa ya mapafu hali iliyopelekea kulazwa hospitali.

Kwa mujibu wa msemaji wa bondia huyo, Bw. Bob Gunnell aliiambia tovuti ya Daily Mail kwa njia ya simu kwamba Muhammad Ali amekuwa akipatiwa matibabu na jopo lake la madaktari na hali yake imeimarika.

”Alikwenda hospitalini asubuhi hii” alisema Gunnel na kuongeza ”alishikwa na nimonia kali na kufanyiwa vipimo vizuri”

Hata hivyo msemaji huyo aligoma kutaja hospitali aliyokuwa amelazwa bondia huyo kutokana ombi la familia kutaka jambo hilo liwe la faragha.

Mara ya mwisho Ali alionekana katika Umma mnamo mwezi Septemba alipohudhuria sherehe katika mji aliozaliwa wa Louisville kwenye utoaji wa Tuzo za Muhammad Ali Humanitarian.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s