EPL : MAN UNITED YALAZIMISHWA SARE YA 1 – 1 NA ASTON VILLA

Falcao aklishangilia bao alilofunga la kusawazisha dhidi ya Aston Villa

Falcao aklishangilia bao alilofunga la kusawazisha dhidi ya Aston Villa

Klabu ya Manchester United al-maarufu kama Mashetani wekundu wakiwa ugenini wamelazimishwa sare ya bao 1 – 1 na Aston Villa katika mtanange uliochezwa kwenye dimba la Villa Park usiku wa leo(Dec.20).

Aston Villa ndio waliokuwa wa kwanza kuliona lango la United kupitia mshambuliaji wake Christian Benteke kabla ya Radamel Falcao kusawazisha mnamo dakika ya 53′ ya kipindi cha pili cha mchezo.

Mchezo mwingine ni ule uliowakutanisha Manchester City waliowakaribisha nyumbani Crystal Palace kwa kuwapa kipigo cha bao 3 kwa mtungi kupitia mshambuliaji wake hatari ‘David Villa’ aliyetupia goli mbili pamoja na goli moja lililofungwa kiungo wa Ivory Coast Yaya Toure.

Kwa matokeo hayo yanaiweka Manchester United nafasi ya 3 ikiwa na jumla ya alama 32 nyuma ya mahasimu wake Chelsea na Man City zenye alama 39 kila moja.

Benteke

Mshambuliaji wa Aston Villa Christian Benteke akishangilia baada ya kuipatia timu yake bao la kuongoza

 

Benteke akipongezwa na wachezaji wenzake wa Aston Villa

Benteke akipongezwa na wachezaji wenzake wa Aston Villa

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s