THIERRY HENRY ATANGAZA KUTUNDIKA DALUGA

 

Thierry Henry

Thierry Henry

Mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa aliyekuwa akikipiga kwenye kikosi cha washika mtutu wa jiji la London, Thierry Henry ametangaza rsami kustaafu soka  baada ya kumaliza mkataba na klabu ya New York Red Bulls inayoshiriki ligu kuu nchini marekani.

Akiwa amekwisha chezea vilabu mbalimbali tajiri ikiwemo Barcelona, Juventus, Monaco,  Arsenal na Red Bulls, Henry mwenye umri wa miaka 37 anakuwa mchezaji wa Historia wa klabu ya Arsenal kwa  kuifungua magoli mengi timu hiyo yapatayo 228 ukitoa 175 ya ligi kuu ya England.

Mbali na kustaafu, Thierry Henry amepata shavu la kuwa mchambuzi wa masuala ya soka kwenye kituo cha Sky Sports akiungana na wakongwe wenzake ambao ni  Gary Neville pamoja  na Jamie Carragher.

Henry atakumbukwa kwa umahiri wake wa upachikaji mabao sambamba na kuwa mshambuliaji hatari aliyepata kusumbua katika ligi kuu ya England(EPL) katika kipindi cha miaka 8 alichoichezea klabu ya Arsenal chini ya kocha mkuu Arsene Wenger.

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s