NICKI MINAJ AMLILIA EX WAKE

Nicki Minaj na Ex Wake  Safaree Samwel

Nicki Minaj na Ex Wake Safaree Samwel

Rapa wa Young Money, Nicki Minaj huwa hapendelei kabisa kuongelea masuala ya mahusiano yake ya kimapenzi, lakini hivi karibuni alishindwa kuvumilia na kutamka wazi kuwa bado ana mapenzi tele kwa mpenzi wake wa zamani licha ya kupigana chini.

Akizungumza na mtangazaji machachari wa Power 105.1, Angie Martinez juu ya kuvunjika kwa penzi baina yake na laaziz wake wa muda mrefu anayefahamika kwa jina la Safaree Samwel, Minaj alinukuliwa akisema…..

”Uhusiano wangu ulikuwa umeegemea katika upendo” na kuongezea ”kulikuwa hakuna kitu chochote zaidi ya upendo”.Haukuwa uhusiano wa mtu niliyekutana nae mtaani. Huyu ni mtu ambae nimekua nae. Ni kama vile sijui nitaweza kuishi vipi bila yeye. kamwe sijawahi kuishi maisha yangu kama staa pasipokuwa yeyealisema Nicki Minaj.

Minaj alienda mbele zaidi kwa kukiri ya kwamba kazi yake ya muziki imechangia kwa kiasi kikubwa kwa penzi lao kwenda mrama.  ”Kama nisingekuwa Rapa, tungelikuwa na watoto, tungelifunga ndoa, na kuishi maisha ya furaha. hicho ndicho kinatusikitisha kwa sababu tunajua kwamba hicho kitu(Muziki) ndio kimesababisha” alisema Minaj.

Hivi karibuni mitandao mingi inayoandika habari za udaku ilimripoti Minaj kutoka kimapenzi na Rapa wa Philly, Meek Mill licha ya mwenyewe kukanusha vikali na kudai kuwa mbali na kushirikiana kimuziki wao ni marafiki wa kawaida.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s