TANZIA : MNENGUAJI AISHA MADINDA AFARIKI DUNIA

 

Aisha Madinda

Marehemu Aisha madinda enzi za uhai wake

Aliyekuwa mnenguaji mahiri wa bendi ya Twanga Pepeta na Extra Bongo, Aisha Madinda amefariki dunia leo katika Hospitali ya Mwananyamala, jiji Dar es Salaam.

Taarifa  kutoka kwa watu wa karibu wa Aisha zinasema kuwa mnenguaji huyo alifika hospitalini hapo kwa ajili ya matibabu na mauti kumkuta hapo hapo hospitalini huku sababu za kifo chake zikiwa bado hazijafahamika.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mwananyamala, Dk. Sophinias Ngonyani alithibitisha kifo hicho na kuongeza kuwa wauguzi waliuona mwili wa marehemu ukiwa hospitalini hapo na kutoa taarifa ambapo ulichukuliwa na kuhifadhiwa kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi.

“Hatujafahamu amekufa kwa ugonjwa gani kwasababu hadi mauti yanamkuta alikuwa bado hajapokelewa na kupatiwa huduma’‘, Aisha pamoja na huyo rafiki yake wamekuwa wakihudhuria hospitalini hapa mara kwa mara kwa ajili ya matibabu maalum,” alisema Dk Ngonyani.

Aisha anatajwa kuwa miongoni mwa wasanii wanaopata matibabu ya kuondoa Uraibu wa matumizi ya dawa za kulevya.

Habari kwa hisani ya Mwananchi.co.tz

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s