YAYA ALIYEMKATILI MTOTO UGANDA APANDISHWA KIZIMBANI

Jolly

Pichani ni mfanyakazi wa ndani ‘Jolly Tumuhiirwe’ akiwa kizimbani nchini Uganda

Mfanyakazi wa ndani nchini Uganda(Yaya) aliyetokea kupata kiki kubwa katika vyombo mbalimbali vya habari Duniani kutokana kitendo chake cha kumpiga mtoto wa bosi wake, hatimaye amepandishwa kizimbani na kukiri juu ya ukatili alioufanya.
 
Msichana huyo aliyetajwa kwa jina la ‘Jolly Tumuhiirwe’ mwenye umri wa miaka 22 huenda akakumbana na adhabu ya kwenda jela miaka 15 endapo atapatikana na hatia.

Tumuhiirwe ambaye alifanya kazi ya ndani kwa mwajiri wake huyo kwa muda wa wiki mbili, alifichuliwa uovu wake kupitia kamera ya siri iliyofungwa nyumbani kwa bosi wake kumrekodi akimkatili kwa kumpiga vibaya mtoto Arnella aliyekuwa na umri wa miezi 18 tu.

Baada ya kukamatwa kwake, polisi nchini Uganda walisema Tumuhiirwe atashtakiwa kwa jaribio la mauaji, lakini mahakama iliyopo katika mji mkuu wa Uganda Kampala imesema mfanyakazi huyo atakabiliwa na shtaka la kumtesa mtoto peke yake.

Yaya UG

Jolly akimpa kipigo mtoto wa mwajiri wake

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s