WIVU WA MAPENZI WASABABISHA RAPA ‘EARL HAYES’ AKATISHE UHAI WAKE NA WA MKEWE ‘STEPHANIE MOSELEY’

Stephanie Mosleye

Marehemu Stephanie Moseley enzi za uhai wake

Mnenguaji wa kimataifa na staa wa kipindi cha”Hit The Floor” kinachorushwa na kituo cha VH1, Stephanie Moseley amefariki Dunia asubuhi ya jana(Dec.08) baada ya kuuliwa kwa kupigwa risasi na mume wake Rapa Earl Hayes na kisha nae kujiua.

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, umemripoti bondia Floyd Mayweather kuwa shuhuda wa tukio hilo kufuatia marehemu Hayes  kumueleza nia yake ya kutaka kukatisha uhai wa mkewe kwa kutokuwa mwaminifu kwenye uhusiano wao.

Hayes

Marehemu Earl Hayes wa kwanza kushoto katika pozi na wanachama wa The Money Team akiwemo Bondia Floyd Mayweather Jr wa kwanza kulia mnamo mwezi March mwaka huu

Kwa bahati mbaya juhudi za Mayweather za kumkataza marehemu kufanya kitendo hicho hazikuweza kuzaa matunda na badala yake alifanikiwa kutimiza dhamira yake.

Kwa nyongeza Rapa Earl Hayes alikuwa akifanya kazi zake chini ya lebo ya mayweather ijulikanayo kama ”The Money Team” wakati kwa upande wa ‘Stephanie Moseley’ alijizolea umaarufu mkubwa kwa kushiriki kama mnenguaji kwenye video za mastaa nyota mbalimbali kama vile Usher, Jennifer Lopez, Chris Brown, Eve, Mariah carey pamoja na Beyonce.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s