IDRIS AIBUKA MSHINDI WA SHINDANO LA BIG BROTHER HOTSHOTS

Idris akishangilia kwa furaha baada ya kutangazwa mshindi wa BBA Hotshots

Kijana mtanashati kutoka Tanzania, Idris Sultan amefanikiwa kuipeperusha vyema bendera ya nchi yake kwa kutawazwa kuwa  mshindi wa shindano la Big Brother Hotshots lililofikia tamati yake usiku wa jana(Nov 7) nchini Afrika kusini baada ya kukaa mjengoni kwa takribani siku 63 ambazo ni sawa na miezi miwili pasipo kutoka nje.

Idris alifanikiwa kumgaragaza mpinzani wake raia wa Nigeria, Tayo aliyeingia nae katika fainali ya shindano hilo kwa kupigiwa kura nyingi zaidi  na mashabiki wake zilizomuwezesha kunyakua kiasi cha dola za marekani 300,000 ikiwa ni sehemu ya zawadi kwa mshindi wa kwanza kama ilivyotangazwa hapo awali.

Mashabiki, wadau na watu mashuhuri kupitia mitandao ya kijamii kama vile Twitter, Facebook na Instagram wamempongeza Idris kwa ushindi sambamba na kuliwakilisha ipasavyo Taifa la Tanzania. 

Tazama hapo chini  picha zaidi za matukio yaliyojiri hapo jana ndani ya mjengo wa BBA

Big-Brother-Hotshots-BellaNaija-December-20142

Idris akiwa shangilia kwa hisia kali ushindi wake

Big-Brother-Hotshots-BellaNaija-December-2014006

Idris wa pili kushoto akipongezwa na washiriki wenzake kwa kuibuka mshindi

Big-Brother-Hotshots-BellaNaija-December-2014007

Idris akihojiwa mara baada ya kutawazwa kuwa mshindi

Big-Brother-Hotshots-BellaNaija-December-2014009

Idris akishika kioo kinachoonyesha dola laki 300,000 za kimarekani alizoshinda

Big-Brother-Hotshots-BellaNaija-December-20140010  Big-Brother-Hotshots-BellaNaija-December-20140013 Big-Brother-Hotshots-BellaNaija-December-20140022 Big-Brother-Hotshots-BellaNaija-December-20140032 Big-Brother-Hotshots-BellaNaija-December-20140042

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s