DRAKE ADAIWA KUSAMBARATISHA PENZI LA CHRIS BROWN NA KARRUECHE

CB, Karrueche & CbMakubwa yamezidi kufichuka juu ya kuvunjika kwa uhusiano wa kimapenzi baina ya mwanamuziki wa miondoko ya R&B kutoka mamtoni(marekani) Chris Brown na mchumba wake Karrueche Tran huku kila mmoja akimtupia lawama mwenzie kwa kuchepuka katika nyakati tofauti.

Kwa upande wa Chris brown amemtuhumu mpenzi wake huyo kuchepuka na hitmaker wa ”Started from the bottom”, Rapa Drake kipindi alipokuwa akitumikia kifungo cha miezi 4 jela na kudai kuwa alikuwa akitumia mwanya huo  kusafiri  jijini Toronto nchini Canada kuponda raha na rapa huyo.

Itakumbukwa usiku wa Nov 05, Chris Brown alitamka hadharani kuwa ni single boy mbele ya umati wa mashabiki wakati akitumbuiza kwenye tamasha la ”Cali Christmas” baada ya kunukuliwa akisema I’m single too, f*ck that b*tch.

Hata hivyo mwanadafada Karrueche ametumia ukurusa wake Instagram kujibu tuhumu hizo na kudai ya kwamba pindi mambo mabaya yanapotokea, unaweza ukayafanya yakuangamize, ya kufafanue au ya kuimarishe.

Karrueche anakuwa mwanamke wa pili kugawa penzi kwa Chris Brown na Drake ukiachia mbali Rihanna ambaye nae aliwahi kuvunja nao amri ya sita mpaka kupelekea kuzuka kwa bifu  kati yao lililodumu kwa takribani miaka miwili.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s