SAKATA LA ESCROW !!!! MAHAKAMA KUU YAZUIA MJADALA WA RIPOTI YA AKAUNTI YA TEGETA ESCROW

Mwananchi

Jopo la majaji watatu wa mahakama kuu kanda ya Dar es salaam chini ya jaji Radhia Sheikh imezuia mjadala wa ripoti ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali kuhusu akaunti ya Tegeta Escrow hadi hapo hoja ya msingi ambayo ipo mahakamani itakapofanyiwa kazi.

 Jopo hilo limeagiza kwa kutokufanyika kwa mjadala wowote kuhusu ripoti ya CAG huko Bungeni na kuongeza kuwa majadiliano hayo yanaweza kufanyika baada ya shauri la msingi mkupatiwa ufumbuzi.

 Awali akizungumza na waandishi, Mwanasheria wa IPTL wakili Joseph Makandege amesema wamefikisha shauri hilo namba 50 katika mahakama hiyo wakitaka vifanyike vitu viwili, kwanza kupata tafsiri sahihi ya kisheria kuwa kama kitendo kilichofanywa na ofisi ya CAG kufanyiwa ukaguzi katika akaunti ya Escrow kama ni sahihi.

 Pili kwa sababu jambo hilo lilikuwa limekwisha amuriwa kisheria na mahakama ilikuwa hakuna haja tena ya bunge kuagiza kufanyike uchunguzi, aidha mwanasheria huyo akaongeza hawataki jambo hilo kujadiliwa Bungeni bali wanataka taratibu zifatwe ili kuweza kufikia muafaka katika jambo hilo.

 Mwanasheria huyo akasema pia wao wanaona kama likijadiliwa bungeni haki haitaweza kutendeka kwa sababu wao kama IPTL hawana muakilishi bungeni hivyo maamuzi yatafanyika upande mmoja.

 Kwa upande wa jopo la wanasheria wa serikali wakiongozwa na Obadia Kaemela wameiomba mahakama kuwapa muda wa kuweza kuwasiliana na baadhi ya watu kama taasisi zinazohusisha katika jambo hilo ili kuweza kupata muda wa kutosha kutoa utetezi wao.

 Kutokana na hali iyo imeamuliwa kuwa baada ya kuwasilishwa kwa taratibu zote ikiwemo uwasilishwaji wa viapo ndipo hapo itakapoanza kusikilizwa Decemba 02 mwaka huu katika mahakumu kuu jijini Dar es salaam.

 Chanzo : ITV

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s