MASTAA NYOTA WA MAREKANI WAIUNGA MKONO FAMILIA YA MAREHEMU MIKE BROWN

A1Mastaa nyota wa fani mbalimbali nchini Marekani akiwemo Rihanna, Katty Perry, Solange, Ciara, Swizz Beatz, Keke Palmer, Alicia Keys na waandamanaji wengine wameiunga mkono familia ya marehemu Mike Brown(18) kwa kupinga maamuzi yaliyotolewa na mahakama ya kumuachia huru afisa polisi mzungu ‘Darren Wilson’ aliyehusika katika mauaji ya Brown yaliyotokea August 9 mwaka huu eneo la Ferguson katika jimbo la Missouri.

Itakumbukwa Mwezi February mwaka 2012 tukio la kuuwawa kwa kijana mweusi ‘Trayvon martin’ lilivuta hisia za watu wengi na vyombo vya habari kufuatia maamuzi yaliyotolewa na mahakama dhidi ya mtuhumiwa wa mauaji hayo ‘George Zimmerman’ huku idadi kubwa ya watu weusi wakilalamikiaupendeleo unaotolewa kwa watu weupe ukilinganisha na hukumu wanazopewa watu weusi pindi wanapofanya matukio yanayofanana na hayo.

Hii sio mara ya kwanza kutokea kwa matukio kama haya yanayotajwa kuchochea ubaguzi wa rangi hasa kutokana na hukumu wanazopewa watuhumiwa ambao ni wazungu ukilinganisha na ukubwa wa tukio lenyewe.

Tazama hapo uone jinsi mastaa hao walivyofunguka kuhusiana na ishu ya Brown kupitia akunti zao za mitandao ya kijamii ya Facebook, Instagram pamoja na Twitter.

  Tweets Tweets1 Tweets2Instagram1Instagram

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s