RAPA NYOTA WA MAREKANI AHUKUMIWA KUNYONGWA MAPEMA MWAKANI

Cool CNi majonzi kwa wapenzi na wadau wa muziki wa Hip-Hop Duniani kufuatia Rapa mkubwa wa marekani, Christopher Roney AKA Cool C aliyewahi kutamba miaka ya 90 kupewa adhabu ya kunyongwa baada ya kukutwa na hatia ya kuhusika katika mauaji ya ofisa mmoja wa polisi yaliyotokea mwaka 1996 mjini Philadelphia.

Kwa mujibu wa taarifa zinasema kwamba Gavana wa Pennsylvania, Tom Corbett amesaini kibali kwa ajili ya Rapa huyo kunyongwa mapema January 08 mwakani. 

Licha ya kukaa mahabusu kwa takribani miongo miwili, Rapa Cool C amekutwa na hatia ya mauaji ya afisa polisi Lauretha Vaird wakati walipovamia benki.  Vaird alikuwa afisa polisi wa kwanza mwanamke kuuwawa mjini Philadelphia akiwa kwenye majukumu yake ya kikazi.

Cool C alijipatia umaarufu mkubwa katika medani ya muziki wa Hip-Hop enzi hizo kupitia ngoma yake ya ”Juice Crew Dis”  iliyotoka mwaka 1989  akiwa kinara wa kundi lililofahamika kwa jina la C.E.B

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s