PICHA ZA MIILI YA WATU 28 WANAODAIWA KUUWAWA NA WANAJESHI WA AL-SHABAAB NCHINI KENYA

Miili ya abiria 28 waliouwawa na wanamgambo wa Al-Shabaab

Miili ya abiria 28 waliouwawa na wanamgambo wa Al-Shabaab

 

Mfululizo wa matuko ya kigaidi bado umeendelea kuiandama nchi ya Kenya baada ya watu wanaodaiwa kuwa ni wanamgambo wa kiislamu wa kundi la Al – Shabab kuwauwa kwa risasi abiria wapatao 28 waliokuwa wakisafiri kwenye basi katika eneo la Mandera mpakani mwa Kenya na Somalia Juzi Jumapili(Nov 22).

Akithibitisha kutokea kwa shambulio hilo, Naibu Kamishna wa Mandera mashariki Elvis Korir alisema taarifa za awali zilionyesha kuwa juu ya wanamgambo 100 wenye silaha walisimamisha basi na kuamuru abiri wote watoke nje.

Alisema shambulio lilitokea wakati basi likipanda mlima mashariki mwa eneo la  Mandera  katika kata ya Arabiya kabla ya kuamriwa kushuka na kisha kuwagawanya katika makundi mawili, ya wasomalia na wasio wasomalia.

”Tunaambiwa watu zaidi ya ishirini na nane wameuwawa na wengine wengi kujeruhiwa lakini sisi bado tutahitaji kujua mpaka pale tutakapopeleka kikosi cha wanausalama katika eneo la tukio” alisema Korir.

Chanzo kingine cha habari kimeeleza kwamba wanamgambo hao waliwagawa makundi mawili, wale waislamu na wasio waislamu na kuwamininia risasi za kichwa ambao hawakuwa waislamu na kisha kutokomea nchini kwao.

 

1897755_592912860835622_8193104543976932951_n

Pichani ni wanajeshi wa Kenya wakiwa eneo la Tukio wakitazama miili ya abiria waliouwawa

10469044_592912594168982_6521832036608081035_n

Basi lililotekwa na wanamgambo wa Al-Shabaab

 

Advertisements

One thought on “PICHA ZA MIILI YA WATU 28 WANAODAIWA KUUWAWA NA WANAJESHI WA AL-SHABAAB NCHINI KENYA

  1. Hiyo adha na shida wanayokutana nayo ndugu Wakenya ina uzembe ndani yake wa viongozi wa juu wa serikali ya Kenya. Haiwezekana huu mwaka wa tatu au nne Raia wae wanauwawa na kuteseka kila wakati, inafikia Hatua watu hawana amani kabisa, Serikali hiyohiyo Kenya juzi tu iliendelea kufanya utumbo hata kwa wasafiri na Madereva wa Kitanzania waliokuwa wakiingia Kenya, sijui wana mtazamo wa namna gani ila hawako makini ktk maamuzi yao au utekelezaji wao ktk kushugurikia matatizo ya ndani na nje ya Kenya.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s