GEEZ MABOVU AFARIKI DUNIA MKOANI IRINGA

Geez Blogu ya Larrybway91 imepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa za kifo cha Rapa maarufu nchini, Geez Mabovu ambaye amefariki Dunia nyumbani kwao alipozaliwa mkoani Iringa alipokwenda wiki chache zilizopita.

Kwa mujibu wa mtandao wa Bongo5, umeeleza kwamba Mabovu alifikwa na umauti baada ya kuugua mfululizo na kuongeza kuwa marehemu anatarajiwa kupumzishwa katika makazi yake ya milele siku ya Alhamisi.

Wadau na mashabiki wa muziki wa Hip-Hop wameendelea kutoa salamu za pole kwa familia ya marehemu. 

Mabovu atakumbukwa kwa ustadi wake wa kuimba, kushambulia jukwaa na kuachia ngoma kali ikiwemo ya ”mtoto wa kiume” ambayo ilitokea kuwabamba sana mashabiki kipindi hicho.

Bwana ametoa, Bwana ametwaa, Mungu aiwekee roho ya marehemu pema peponi Ameeen

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s