BIRDMAN AINGILIA KATI BIFU LA DRAKE NA TYGA

birdmanMwanzilishi na mmiliki wa lebo ya YMCMB, Bryan Adams AKA Birdman amefunguka kwa mara ya kwanza juu ya bifu la Drake na Tyga pamoja na madai yaliyotolewa na hitmaker huyo wa Racky City kupitia ukurasa wake wa Twitter kuhusu kutaka kuihama lebo hiyo kwa kile alichodai kucheleweshwa kutoka kwa albamu yake mpya inayokwenda kwa jina la Gold Album.

Wakati wa mahojiano na mtangazaji Funkmaster Flex wa Hot 97, Birdman alikiri wazi kushangwazwa na tweets za Tyga.

Itakumbukwa ya kwamba Tyga alinukuliwa katika moja ya mahojiano yake aliyofanyiwa na jarida la Vibe akitamka wazi kuwa hampendi Drake na Nick minaj.

“Binafsi simpendi Drake. Yeye ni mnafki kwangu” ,alisema Tyga.

Katika kuweka mizani sawa, Birdman alionekana akimkingia kifua Drake kwenye mahojiano na Flex.

“Drake ni Drake. Hakuna kumlinganisha. Yupo vizuri pindi linapokuja suala la kutoa ngoma kali. Huwezi kumlinganisha na mtu yoyote kwa kile anachokifanya na mtu yoyote anafanya kile anachoweza fanya “ .alisema Birdman na kuongezea “Tyga anafahamu sehemu alipo kwenye hili gemu la muziki ukimlinganisha na Drake. Hilo halina siri. Namba haziongopi. Yeye anaweza kuwa kwenye hisia zake, na nina upendo na heshima kwa Tyga”

Pia Birdman amempa nafasi Tyga ya kuchagua  kubaki au kuondoka katika lebo ya YMCMB kwa kile alichodai kwamba hawezi kujihusisha katika bifu lao.

“Sipo katika bifu hilo, sipo upande wowote. Sisi ni familia. Hakuna kitakachotutenganisha. Iwe umehusika au lah. Unaweza ukachagua upande wako “. alisema Birdman.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s