PICHA : POLISI WASHAMBULIA WAANDISHI WA HABARI WAKITAWANYA WAFUASI WA CHADEMA

IMG_9743

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Freeman Mbowe akiwasili kwenye makao makuu ya Jeshi la Polisi nchini,Mapema leo asubuhi tayari kwa kwenda kuhojiwa juu kauli aliyoitoa kwenye Mkutano Mkuu wa chama hicho hivi katibuni,kuwa watafanya maandamano nchini nzima bila kikomo.

Siku moja baada ya makamu wa rais dkt mohamed ghalib bilal kuhimiza mahusiano mema wakati wa utendaji kazi baina ya vyombo vya ulinzi na usalama na vyombo vya habari, jeshi la polisi likiwa na silaha pamoja na mbwa limekiuka kauli hiyo kwa kuwapiga na kuwajeruhi baadhi ya waandishi wa habari na kuwazuia kutekeleza wajibu wao wakati mwenyekiti wa Chama cha demokrasia na maendeleo Chadema alipowasili katika makao makuu ya jeshi hilo kwa mahojiano.

Kauli hiyo ya makamu wa rais imeshindwa kutekelezwa kutokana na tukio lililotokea majira ya saa 5 na dk 15 asubuhi wàkati mwenyekiti wa chadema taifa Mhe. Freeman Mbowe alipowasili makao makuu na askari wa polisi  kutaka kuzuia gari alilopanda kuingia ndani ya lango kuu pamoja na waandishi wa habari na watu wengine kuamriwa kuondoka katika eneo hilo agizo lililopingwa na waandishi wa habari na baadhi ya wanasheria wa Chadema.

Kufuatia na kutolewa kwa ilani hiyo jeshi la polisi kikosi cha kutuliza ghasia-FFU- kilianza kupiga waandishi wa habari pamoja na baadhi ya wananchi huku wengine wakikimbia kuhofu vipigo toka kwa askari hao ambapo baaadhi ya waandishi walioumizwa sehemu mbalimbali ya mihili yao.

Akiwatangazia wafuasi waliokuwa wakikataa kuondoka katika maeneo hayo mwanasheria wa chadema mhe. Tundu lissu licha ya kuwahakikishia kuwa mwenyekiti wa chama hicho taifa Mhe. Freeman Mbowe yuko salama amewataka kuondoka katika eneo hilo na kurudi majumbani ili kuepusha vurugu na misongamano ambayo ingeweza kusababisha matatizo zaidi.

Aidha ITV imeshuhudia mwenyekiti wa Chadema taifa Mhe Freeman Mbowe akitoka makao makuu ya jeshi la polisi akisindikizwa na ulizni mkali wa jeshi la polisi kuelekea katika ofisi za makao makuu ya chama hicho baada ya kukamilika kwa taratibu za kipolisi.

 

10408762_571771142952529_1753592868089723026_n

Wafuasi wa Chadema wakimsindikiza mwenyekiti wao Freeman Mbowe kuelekea Makao makuu ya jeshi la polisi

Pix 1.

Wafuasi wa CHADEMA wakimpokea mwenyekiti wao, Freeman Mbowe baada ya kuwasili makao makuu ya polisi

10360248_298425287015760_2395346902320766670_n

Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA John Mnyika akizungumza na waandishi wa habari waliokuwepo kwenye eneo la makao makuu ya Jeshi la Polisi,juu ya kile kilichokuwa kikiendelea kwenye mahojiani katika ya Mwenyekiti wa Chama hicho na Jeshi la Polisi.

10671469_571771159619194_7364080053767316705_n

Wafuasi wa CHADEMA wakielekea makao makuu ya jeshi la Polisi

10672414_527065064104880_3421463650254803815_n

Waandishi wakipewa mkong’oto na askari wa kikosi cha FFU

10678742_705905146125658_9140054834563609414_n

askari wa kike wa kikosi cha FFU

10701992_527065057438214_6761671076172324404_n

Polisi wakiwa na mbwa wa kutuliza ghasia nje ya makao makao makuu ya polisi jijini Dar es salaam

DSCF9030

Naibu katibu wa CHADEMA, John Mnyika akizungumza na waandishi wa habari

IMG_0200

Huyu alikuwa akikaidi amri ya Jeshi la Polisi ilibidi aondolewe kwa nguvu.

IMG_9523

Makamu Mwenyekiti wa Chadema,Prof. Abdallah Safari na Wakili wa Chama,Wakili Mabele Marando wakiwasili kwenye Makao Makuu wa Jeshi la Polisi.

Pix 3.

Mwenyekiti wa Chama cha DP, Christopher Mtikila akihojiwa na askari Polisi, alipowasili Makao Makuu ya Polisi jijini Dar es Salaam kwa kutumia usafiri wa bajaji, ambako Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe alihojiwa na Polisi.

       IMG_0276 IMG_0336 IMG_0471 IMG_9552   Pix 4. Pix 5.

Chanzo : ITV

 

Advertisements

One thought on “PICHA : POLISI WASHAMBULIA WAANDISHI WA HABARI WAKITAWANYA WAFUASI WA CHADEMA

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s