MATOKEO YA MECHI ZILIZOPIGWA JANA(SEPTEMBA 17) KLABU BINGWA ULAYA

Jerome Boateng akishangilia baada ya mchezo kumalizika na kufanikiwa kuipatia timu yake pointi tatu muhimu dhidi ya City

Jerome Boateng akishangilia baada ya mchezo kumalizika na kufanikiwa kuipatia timu yake pointi tatu muhimu dhidi ya City

Mchakamchaka wa ligi ya mabingwa barani Ulaya bado umeendelea usiku wa jana baada ya Bayern Munich ikiwa nyumbani kuipa dozi ya bao 1 – 0 Manchester City katika kundi E.

Goli pekee na la ushindi kwa Bayern liliifungwa na Jerome Boateng mnamo dakika ya 90′  huku wachezaji wanne wakutumainiwwa wa  City akiwemo Edin Dzeko, Vicent Kompany, Gael Clichy pamoja na Martin Demichelis wakijikuta wakimaliza mchezo huo kwa kupewa kadi ya njano kila mmoja.

Mchezo mwingine wa Kundi E ulikuwa kati ya Roma waliowapa kipigo goli 5 – 1 CSKA ya Moscow kupitia wachezaji wake Juan Manuel Iturbe, Gervinho aliyetupia mawili, Maicon na goli moja la kujifunga toka kwa Sergei Ignashevich wa CSKA.

Miamba ya Hispania, Barcelona walifanikiwa kunyakua pointi tatu muhimu na kuongoza kundi F baada ya kuitungua goli 1 – 0 Apoel Nicosia, goli lililofungwa na beki Gerard Pique mnamo dakika ya 28 ya kipindi cha kwanza cha mchezo.

Ajax na Paris St.Germany walijikuta wakienda sare na  kugawana pointi moja moja baada ya kutoka sare ya 1 – 1 magoli yaliyofungwa na Edinson Cavani wa PSG kabla ya kurudishwa na Lasse Schoene wa Ajax.

Huku watoto wa darajani, Chelsea ”The Blues” wakishindwa kuonyesha uwamba wao kufuatia kulazimishwa suluhu ya 1 – 1 na Schalke 04 ya Ujerumani licha ya Cesc Fabregas kuwa wa kwanza kuzifumania nyavu zao kabla ya Klaas Jan Huntelaar kusawazisha kipindi cha pili.

Mtanange mwingine uliokuwa wa kukatana na shoka kwa jana ni ule uliowakutanisha FC Porto ya Ufaransa iliyowaangushia kiama cha mabao 6 kwa nunge BATE BORISOV.

Yasine Brahimi wA Porto alifanikiwa kuondoka na mpira baada ya kutupia goli tatu peke yake akifuatiwa na wachezaji wenzake Jackson Martinez, Adrian pamoja na Vicent Aboubakar ambao walifunga goli moja moja.

 

 

 

 

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s