MATOKEO YA MECHI ZA UFUNGUZI KLABU BINGWA ULAYA

Carlos Teves akishangilia goli alilofunga la kuongoza dhidi ya Malmo

Carlos Teves akishangilia goli alilofunga la kuongoza dhidi ya Malmo

Kitimtimu cha klabu bingwa Ulaya ”UEFA Champions League” kimeanza rasmi kutimua vumbi hapo jana Septemba16 katika viwanja mbalimbali, kwa upande wa kundi A ambalo liliwakutanisha vibibi vizee wa Turin, Juventus waliowapa kipigo cha bao 2 – 0 Malmo FF huku Magoli yote mawili ya Juve yakifungwa na Carlos Tevez katika kipindi cha pili mnamo dakika ya 59′ na 90′.

Mchezo mwingine wa kundi A ulikuwa kati ya Olympiakos walioipa kipigo cha bao 3 – 2 Atletico madrid, magoli ya Olympiakos yakifungwa na Arthur Masuaku, Inrahim Afellay na Konstantinos Mitroglou huku magoli mawili ya Atletico  yakifungwa na Mandzukic pamoja na Antonie Griezmann.

Straika wa Olympiacos, Kostas Mitroglou akishangilia baada ya kufunga bao dhidi ya Atletico Madrid

Straika wa Olympiacos, Kostas Mitroglou akishangilia baada ya kuifungia timu yake bao la kuongoza dhidi ya Atletico Madrid

Majogoo wa jiji la London, Liverpool walianza vyema katika kundi B kwa kuinyuka goli 2 – 1 PFC Ludogorets Razgrad kupitia wachezaji wake hatari, Mario Balotelli na  Steven Gerrard.

Real Madrid nao wakiwa nyumbani waliweza kuiangushia mvua ya magoli 5 – 1 Basle. Gareth Bale, Cristiano Ronaldo, James Rodriguez, Karim Benzema na goli la kujifunga toka kwa Marek Suchy yaliweza kuipa pointi tatu muhimu za kundi B  miamba hiyo ya Hispania.

Mchezo mwingine uliokuwa na upinzani mkali ni ule wa kundi D uliozikutanisha Borrussia Dortmund ya Ujerumani walioipa kibano cha bao 2 – 0 washika mtutu wa jiji la London, Arsenal.  Mabao ya Dortmund yalifungwa na Ciro Immobile mnamo dakika ya 45′ na Pierre-Emerick Aubameya dakika ya 48′.

Ciro Immobile wa Dortmund akishangilia baada ya kufunga bao la kuongoza dhidi ya Arsenal

Ciro Immobile wa Dortmund akishangilia baada ya kufunga bao la kuongoza dhidi ya Arsenal

 

Bale na Ronaldo wakipongezana baada ya kuilowesha ngome Basle

Bale na Ronaldo wakipongezana baada ya kuilowesha ngome Basle

 

 

 

 

 

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s