KIPOFU KAONA MWEZI : MAN UNITED YAINYUKA 4 – 0 QUEENS PARK RANGERS

1410723445451_wps_20_MANCHESTER_ENGLAND_SEPTEM

Wayne Rooney, Ander Herrera na Angel Di Maria wakisherekea ushindi

Hatimaye kipofu kaona mwezi, klabu ya Manchester United imeweza kuibuka na ushindi mnono wa mabao 4 – 0 dhidi ya Queens Park Rangers ukiwa ni ushindi wao wa kwanza tangu kuanza kwa ligi kuu ya England ‘EPL’ wakiwa chini ya kocha mkuu muholanzi Lousi Van Gaal katika mchezo uliopigwa kwenye dimba la Old Trafford hapo jana Septemba 14.

Bao la kuongoza kwa United liliwekwa wavuni na kiungo hatari wa timu ya Taifa ya Brazil, Angel Di maria mnamo dakika ya 24′ huku la pili likifungwa na Ander Herrera dakika ya 36 kabla ya Wayne Rooney kutupia bao la tatu dakika moja kabla ya angwe ya kwanza kumalizika.

Katika kipindi cha pili kilichokuwa cha vuta nikuvute kiliiwezesha United kuongeza bao lingine la 4 kupitia kiungo mshambuliaji Juan Mata mnamo dakika ya 58 na mchezo kumalizika kwa mashetani wekundu  kuibika na ushindi wa alama 3 za nguvu ikiwa imeshikilia nafasi ya 9 nyuma ya Liverpool kwa jumla ya pointi 5.

1410724639120_wps_26_Manchester_United_s_Angel

Kiungo Angel Di Maria akishangilia kwa hisia goli alilofunga

1410765885698_Image_galleryImage_epa04400566_Manchester_Un

Tyler Blackett akimpongeza Angel Di Maria kwa goli alilofunga na kiwango cha hali ya juu alichoonyesha

 

1410723477002_wps_21_Radamel_Falcao_of_Manches 1410723620159_wps_22_Manchester_United_s_Argen

Advertisements

One thought on “KIPOFU KAONA MWEZI : MAN UNITED YAINYUKA 4 – 0 QUEENS PARK RANGERS

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s