BILL GATES AIPIGA TAFU AFRIKA MAGHARIBI KWA KUCHANGIA DOLA MILIONI 50 KUPAMBANA NA EBOLA

Bill Gates na mkewe Melinda

Bill Gates na mkewe Melinda

Tajiri nambari moja Duniani na muanzilishi wa kampuni ya Microsoft, Bill Gates na mkewe Melinda kupitia mfuko wao wa The Bill & Melinda Gates Foundation wamejitolea kuipiga tafu Afrika Magharibi kwa kuchangia kiasi cha dola za kimarekani milioni 50 ambazo ni sawa na bilioni 80 za kitanzania katika kupiga vita ugonjwa hatari wa Ebola.

Bill Gates na mkewe walitangaza jumatano iliyopita kupitia mtandao wa Twitter kuchangia kiasi hicho kikubwa cha pesa kwa ajili ya kuutokomeza ugonjwa huo hatari ulioshika kasi kwa nchi za Afrika Magharibi.

Habari zinaeleza kwamba kiasi hicho cha hela kinatajwa kuwa ni kikubwa kuwahi kuchangiwa na mifuko ya watu binafsi ambapo awali mfuko huo ulikuwa tayari umeshachangia kiasi cha dola za kimarekani milioni 10.

”Kwa kupambana na Ebola sasa, tunaweza kuhakikisha halitakuwa janga katika Afrika Magharibi”, aliandika Bill Gates kwenye ukurasa wake wa Twitter

Rekodi hiyo inakuja kufuatia maombi yaliyotolewa na katibu mkuu wa umoja wa mataifa Bwana Ban Ki-Moon ya dola milioni 600 kwa ajili ya kupambana na janga hilo ambalo mpaka sasa limeshauwa watu takribani 2000 kutoka Liberia, Nigeria, na Sierra  Leone.

Taarifa kutoka Gates Foundation ilisema: ”Hadi sasa, the Gates Foundation ina nia ya kujitolea zaidi ya dola milioni 10 kati ya dola milioni 50  kupambana na Ebola, ikiwa ni pamoja na dola milioni 5 kwa shirika la afya Duniani(WHO) kwa ajili ya shughuli za dharura na tathimini na dola milioni 5 kwa mfuko wa Marekani kwa ajili ya UNICEF kuunga mkono juhudi  katika kuisaidia Liberia, Sierra Leone na Guinea kununua mahitaji muhimu ya matibabu, kuratibu shughuli za majibu na kuitoa katika hatari jamii na habari za afya”.

Alhamisi ya Septemba 11, Reuters iliripoti kuwa mwanzilishi mwenza wa kampuni ya Microsoft, Paul Allen alikuwa atangaze kwamba angetoa dola milioni 9 kwa kituo cha kudhibiti na kuzuia magonjwa kwa ajili ya kusaidia kupambana na virusi hivyo.

Chanzo : Business Insider

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s