PENZI LA FRENCH MONTANA NA KHLOE KARDASHIAN IMEBAKI STORI

French Montana na Khloe Kardashian

French Montana na Khloe Kardashian

Trouble In Paradise!!! Baada ya kudumu kwenye mahusiano ya  kimapenzi ya nguvu ya soda kwa takribani miezi 8, Rapa mwenye asili ya Morocco, French Montana amepigwa chini na mrembo Khloe Kardashian  kwa amani huku kila mmoja akiongea lake.

Kwa mujibu wa habari zilizotanda kwenye mitandaoni mingi ya udaku zinadai ya kwamba Montana amekuwa tegemezi na kumtumia kimaslahi mpenzi wake huyo ambaye ni staa wa kipindi cha televisheni cha Keeping up with the Kardashian.

Siku chache zilizopita Khloe aliposti ujumbe mzito kwenye ukurasa wake wa Instagram uliotafsiriwa kama dongo kwa Montana ambaye katika kipindi cha mapenzi yao motomoto aliwahi kumzawadia mkoko aina ya Jeep kwenye siku yake ya kuzaliwa.

”maybe one day we’ll find that place where you and i could be together. and we’ll  catch our dreams. so smile for me one last time and believe that we’ll meet again. until then, i ‘ll be missing you”. aliandika Khloe

Awali Khloe anayetokea kwenye familia ya Kardashians alikuwa mke wa mcheza kikapu Lamar Odom kabla ya kuamua kutalikiana kishingo upande mwaka jana kwa kile kilichotajwa kuwa ni usaliti na matumizi ya madawa ya kulevya.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s