PICHA : AJALI YA MABASI YACHINJA WATU 39 NA KUJERUHI 79 MKOANI MARA

4

Wakazi wa Butihama na vitongoji vyake wakishuhudia ajali

 

Watu wapatao 39 wamefariki Dunia papo hapo na wengine 79 kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha mabasi mawili na gari dogo iliyotokea leo asubuhi katika kijiji cha sabasaba wilayani Butihama mkoani Mara.

 Mabasi mawili yaliyohusika katika ajali hiyo yaliyotokea katika barabara ya Musoma – Mwanza ni J4 Express lenye namba za usajili T 677 CYC lilokuwa likitokea Mwanza kwenda Silari mkoani Tarime na basi la Mwanza Coach lenye namba za usajili T 736 AWJ lilokuwa likielekea Mwanza kutoka Musoma.

 Aidha gari dogo lilohusika katika ajali hiyo liligongwa na moja ya mabasi hayo na kutumbukia mtoni katika daraja lililo katika barabara hiyo.

 Maiti na majeruhi katika ajali hiyo wamepelekwa katika hospitali ya rufaa ya Musoma ambako maiti wamehifadhiwa na majeruhi wanatibiwa.

 Akizungumza kwa niaba ya mganga mkuu wa Mkoa wa Mara, Dkt Martin Khan amesema hospitali ya rufaa ya Musoma imepokea maiti na idadi kubwa ya majeruhi ambao wengi wao hali zao si za kuridhisha.

1

Pichani ni basi la J4 Express baada ya kupata ajali na kuharibika nyang’anyang’a

2

Wauguzi wa Hospitali ya Rufaa Mara wakiwa eneo la tukio

3

Basi la Mwanza Coach baada ya kula mzinga

6

Wauguzi wakitoa huduma kwa majeruhi

7

Askari wa usalama barabarani na mapolisi wakiangalia usalama

9

Mizigo ya abiria waliokuwemo kwenye mabasi ya J4 na mwanza Coach

10

Tingatinga likitoa gari dogo mtoni

  5 8 11 12 13 14

Advertisements

7 thoughts on “PICHA : AJALI YA MABASI YACHINJA WATU 39 NA KUJERUHI 79 MKOANI MARA

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s