MCHEKESHAJI JOAN RIVERS AFARIKI DUNIA AKIWA NA MIAKA 81

Joan Rivers

Joan Rivers

Dunia yazizima kufuatia kifo cha mchekeshaji nyota, Joan Rivers aliyefariki Dunia jana(Agosti 04)  saa 7 mchana kwenye hospitali ya Manhattan nchini Marekani akiwa na umri wa miaka 81.

Kifo cha Rivers kimetokana na moyo wake kushindwa kufanya kazi baada ya kufanyiwa upasuaji katika koo kwa ajili ya kurekebisha sauti wiki iliyopita kwenye kliniki moja iliyoko mjini New York.

Idara inayohusika na masuala ya afya jijini New York imetangaza kufanyia uchunguzi kituo hicho kilichomfanyia upasuaji Rivers.

”Kwa majonzi makubwa natangaza kifo cha mama yangu mzazi, Joan Rivers”. alisema mtoto wa marehemu aitwae Melissa Rivers na kuongeza ”amefariki kwa amani akiwa amezungukwa na wanafamilia pamoja na marafiki wa karibu”.

Marehemu  Joan Rivers alijizolea umaarufu mkubwa hasa kutokana na kazi yake ya uchekeshaji na umahiri wake katika utangazaji wa vipindi mbalimbali vya  luningani kama vile  In Bed With Joan. Rivers ameacha mtoto mmoja wa kike aitwaye Melissa Rivers .

Joan Rivers na binti yake Melissa

Joan Rivers katika pozi na binti yake Melissa

 

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s